Na Tiganya Vincent-RS-TABORA

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri ameagiza kuanzia msimu ujao wa kilimo kila mtu mwenye uwezo wa kufanyakazi ni lazima alime heka mbili za alizeti kwa ajili ya kuvutia wawekezaji kujenga Viwanda vya kusindika na kuzalisha mafuta hayo kuanza ujenzi mkoani humo.

Bw. Mwanri alitoa kauli hiyo jana wakati wa ufunguzi wa maonesho ya nanenane kwa Kanda ya mikoa ya Magharibi yaliyofanyika mkoani Tabora.

Alisema zao la alizeti katika mkoani Tabora linastawi sana na ikiwa wakazi wake watalima kwa wingi Kampuni mbalimbali zitajitokeza kwa wingi kuja kujenga viwanda vya kuzalisha mafuta hayo.

Bw.Mwanri alisisitiza kuwa wawekezaji wengi wamekuwa wanashindwa kuja kujenga viwanda vya usindikaji wa mafuta hayo kwa sababu siku za nyuma zao hilo limekuwa halitiliwi mkazo na kufanya uzalishaji kuwa wa chini sana , lakini hivi sasa hiyo itakuwa ajenda ya Mkoa kama mkakati mojawapo wa kuwavutia watu kuja kujenga viwanda.

“Ndugu zangu Wakuu wote wa Wilaya na Wakurugenzi kuanzia sasa akili yetu na agenda yetu kubwa iko katika kuhakikisha kuwa kila mkazi wa Tabora analima heka mbili za alizeti kuanzia msimu ujao wa kilimo ili tuwe na malighafi nyingi kwa ajili ya kulisha viwanda vitakavyoanzishwa kwa mwaka mzima” alisema Mkuu huyo Mkoa.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...