BIA ya Safari Lager inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) inasheherekea miaka 40 tangu kuzalishwa hapa nchini mwaka 1977 ikiwa bia ya kwanza ya Kitanzania. Shamrashamra hizo zitaanza rasmi siku ya Jumamosi 12 Agosti katika viwanja vya Leaders Club ambapo wasanii mbalimbali maarufu watatoa burudani ya muziki.

Akiizungumzia Safari Lager Meneja wa bia ya Safari Lager Bi. Edith Bebwa Nasuwa  alisema kuwa hatua ya mafanikio iliyofikiwa na bia ya Safari ni ya kujivunia na hasa kwa sababu bado inaendelea kuwa moja ya kinywaji kinachopendwa zaidi katika soko lenye chapa nyingi za bia.Safari Lager ni bia inayoongoza kwa tuzo za ubora wa kimataifa hivyo inampa mnywaji thamani ya pesa yake.”

“Ili kuzindua kampeni hii ya kusherehekea miaka 40 ya Safari yetu tumeandaa burudani kabambe zitakazoanzia jijini Dar es Salaam na kuelekea mikoani ili kuwashukuru wateja watu wetu kwawa nasi katika safari hii.”

Tutashuhudia safari ya burudani kutoka kwa wanamuziki mbalimbali katika uzinduzi wa sherehe za miaka 40. Safari ya burudanu itaanzishwa na mwimbaji maarufu Hassani Bichuka akiwa na Ali Choki, wakipiga nyimbo zao na msanii wa kizazi kipya Barnaba na Odama band, wanamuziki wa bongo fleva Sir Juma Nature, Dully Sykes, Ray C na wa kizazi kipya  Joh Makini. Kwa kuongeza burudani kuna maDJ maarufu akiwemo DJ John Dilinga, DJ Zero na DJ Fast Eddie.

“Tunajivunia kuwa nchini kwa miaka 40 na bado Safari lager inatazamia kuwepo miaka 40 ndiyo maana tunasema #40naBaado. Tunawaalika wateja wetu wote na wapenzi wa Safari Lager waje kusheherekea nasi jumamosi, kiingilio ni Safari Lager mbili tu. Tunataka wateja wetu wajivunie na wao kwa hatua hii ya mafanikio kwa sababu wao ndio wadau wetu wakubwa,” aliongezea Edith.

Tunawaambia wakazi  wa miji ya Arusha, Moshi, Mbeya, Tunduma, Tukuyu, Makambako, Mbinga, Babati, Singida, Mtwara, Tandahimba, Nachingwea, Babati na Songea kwani baada ya Dar es Salaam safari hii ya burudani inenda kwao, #40NABAADO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...