ZAWA1
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari – MAELEZO, Bibi. Zamaradi Kawawa akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusiana na taarifa za kuzuiwa kwa ndege ya Serikali aina ya Bombadier ambayo inatengenezwa nchini Canada.  (Picha na: Idara ya Habari – MAELEZO)
ZAWA2
Serikali imethibitisha na kuwahakikishia Watanzania kuwa ujio wa ndege mpya ya tatu aina ya Bombardier Q400-Dash 8 upo pale pale licha ya baadhi ya wanasiasa wasio wazalendo kutumia kila njia kukwamisha ujio huo.

Kauli ya kuthibitisha ujio wa ndege hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Bi. Zamaradi Kawawa wakati akiongea na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam.

Alieleza kuwa kuchelewa kwa ndege hiyo ambayo ilitakiwa kuwasili mwezi Julai mwaka huu kumetokana na majadiliano yanayoendelea ambayo kimsingi yamechangiwa na baadhi ya wanasiasa wasio wazalendo kushiriki kwao moja kwa moja kuweka zuio mpaka pale majadiliano yatakapo kamilika.

“Kuna baadhi ya Watanzania wenzetu wenye maslahi binafsi wanapiga vita ndege hii kuletwa nchini lakini Serikali inawahakikishia wananchi kuwa ndege itakuja na hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi”, alisisitiza Zamaradi.
Alieleza kuwa Serikali iliishapata fununu kuwa kuna kuna baadhi ya viongozi wa chama cha siasa wana mpango wa kukwamisha juhudi za ujio wa ndege mpya na kwamba bila hata chembe ya uzalendo, watu hao wamejidhihilisha wenyewe hadharani kwamba wapo nyuma ya pazia la kuhujumu jitihada za Serikali kwa maslahi yao binafsi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...