THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Shughuli mbalimbali za kilele cha siku ya wakulima nane nane mkoani Ruvuma

 Katibu tawala msaidizi utumishi na utawala katika sekretarieti ya mkoa wa Ruvuma  Bw. Biseko Bwai (kushoto) akiangalia maziwa yaliyosindikwa na mjasilimali mdogo aliyefahamika kwa jina moja la mama Tarimo wakati wa kilele cha siku ya wakulima nane nane mkoani Ruvuma jana.

 Afisa kilimo kutoka halmashauri ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Bw. Jibinza Masaba (kushoto)  akiwaeleza baadhi ya wananchi waliofika katika maonesha ya siku ya wakulima nane nane nyanya ambazo zinaweza kuishi na kuzaa kwa muda wa miezi sita tofauti na nyanya nyingine ambazo zinaishi kwa miezi miwili.
 Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Songea wakiangalia kibao kinachoonesha aina ya mbegu ya ngano na mahindi yenye uwezo wa kutoa gunia 40 kwa ekari moja katika viwanja vya nanenane  wakati wa kilele cha mnaadhimisho ya siku ya wakulima mkoani Ruvuma. Picha na Muhidin Amri