Na Godfrey Robert Malema
Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini  Mhe. Hussein Mohammed Bashe anapenda kuwataarifu umma ya kuwa tayari serikali imetoa fedha kiasi cha Shilingi Milioni Mia Mbili (Tzs 200,000,000) maalum kwa ajili ya kutatua matatizo au kero za maji na miundombinu ya maji ndani ya Jimbo la Nzega Mjini.
Kupatikana kwa fedha hizi ni matokeo ya Mhe. Hussein Bashe kumuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu wakati wa ziara ya kikazi ya Rais mkoani kwetu.
Ili kuhakikisha tunafikia malengo yaliyokusudiwa; Usimamizi wa fedha hizi hautafata taratibu za tenda ila utafuata utaratibu wa kuwa na timu ya pamoja itakayojumuisha Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Ofisi ya Mkurugenzi, Ofisi ya Mbunge, Mamlaka ya Maji, Madiwani wa Kata ya Nzega Mjini Magharibi, Nzega Mjini Mashariki na  Wenyeviti wa Serikali ya Mtaa katika maeneo ambayo yatahusika na ukarabati huu mkubwa.

Aidha; Matumizi ya Fedha hizi yatajumuisha Usafishaji na Ukarabati wa Bwawa la Uchama;  Ukarabati wa Miundombinu ya Maji  ili kusaidia maji kuweza kufika maeneo ya mbali; Ujenzi wa Maghati Matano (5) kutoka Nyasa Mahakamani hadi Stendi Mpya; jambo hili litafanikisha ujenzi wa mtandao mpya wa maji wenye urefu wa zaidi ya mita 200 kupitia mtaa wa Uswilu.
Hivyo; Ofisi ya Mbunge inawataka madiwani wote kushirikiana na Wenyeviti wa serikali za Mitaa kuweza kubaini na kupendekeza maeneo sahihi ya ujenzi wa Maghati haya mapya.
Kipekee kabisa, Mheshimiwa Hussein Bashe anapenda kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa John Pombe Magufuli kwa namna anavyoendelea kushirikiana na wananchi wa Jimbo la Nzega Mjini katika kutatua kero mbalimbali ikiwemo kero na kilio cha muda mrefu juu ya Ukosefu wa Maji.

Na mpaka sasa tayari Rais anakua ametimiza ahadi yake ya kutupatia Tzs 400,000,000 ambazo nilimuomba nyakati tofauti ili kutatua changamoto kubwa za shida ya maji jimboni.
Kwa upande mwingine Mbunge anapenda kuwashukuru Waziri wa Maji Mhe. Gerson Lwenge na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhe. Prof. Kitila Mkumbo pamoja na watumishi wote wa Wizara hii kwa namna ambavyo wamekua wakishirikiana nasi katika kusaidia kupunguza matatizo ya maji ndani ya Jimbo la Nzega Mjini huku tukisubiria kukamilika kwa Mradi Mkubwa wa Maji wa Ziwa Victoria.
Mwisho, Ofisi ya Mbunge inapenda kusisitiza ya kuwa ni wajibu wetu wote kuhakikisha tunalinda vyanzo vyetu vya maji na kutoshiriki kwa namna yeyote katika kuharibu miundombinu ya maji ndani ya Jimbo la Nzega Mjini na mahali popote nchini ili kuvilinda na kuviendeleza vyanzo vilivyopo kwa matumizi endelevu ya kizazi kilichopo na vizazi vijavyo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Siasa ni shida! Kisheria Mbunge ni Diwani hivyo anafanya juhudi ya ufuatiliaji wa kitu inakuwa kwa niaba ya Jimbo na Halmashauri yake. Haiingii akilini Mbunge kusema ana Ofisi kwani Ubunge si Taasisi. Matumizi ya Fedha lazima yafuate Tenda hata km ikiwa ni Force Account bado usimamizi ni muhimu!. Hakika Wakurugenzi wa Sasa ktk LGAs mna kazi kweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...