Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi wa Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS) Dkt. Augustine Massawe akizungumza katika uzinduzi wa Mpango Mkakati wa kusaidia mifumo ya afya wa miaka mitano ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016- 2020. Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mpango Mkakati wa kusaidia mifumo ya afya wa miaka mitano ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016-2020 na Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS).  Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya (wa nne toka Kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Redempta Mbatia (wa tako kutoka kushoto) pamoja na wadau wa afya wakionyesha chapisho la Mpango Mkakati wa kwanza wa kusaidia mifumo ya afya  wa Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS) ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016-2020.
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Health Promotion Support (THPS) inayosaidia Wizara za afya Tanzania Bara na Zanzibar kutoa kinga ya Virusi vya Ukimwi (VVU), huduma, matibabu na msaada kwa kuimarisha mifumo ya afya imezindua mpango mkakati wa kwanza wa miaka mitano.

Akizungumza katika uzinduzi huo wa mpango mkakati uliofanyika Jijini Dar es salaam leo. Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi wa THPS, Dkt. Augustine Massawe alisema mpango mkakati wa kwanza wa taasisi hiyo ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016 mpaka 2020 umelenga kusaidia juhudi za Wizara ya afya, Serikali za mitaa, Washiriki wengine na Wadau kuhakikisha huduma bora za afya zinazoshugulikia afya ya umma ikiwemo magonjwa yanayoambukizwa na yasiyoambukizwa ili kuboresha matokeo ya afya kiujumla katika jamii. 

Dkt. Massawe alisema anatarajia mpango mkakati utazingatia mawazo kati ya wadau muhimu wa THPS na kujenga uamuzi wa pamoja wenye matokeo mazuri. “tunataka kugusa maisha ya Watanzania wengi kwa kuathiri ubora wa huduma za afya na kujenga taifa huru la VVU/UKIMWI. Nina matumaini kuwa mpango mkakati uliofikiriwa utakuwa kama chombo cha usimamizi wa taasisi katika kuweka vipaumbele, kuzingatia nishati na rasilimali, kuimarisha shughuli mbalimbali na kuhakikisha wafanyakazi na wadau wengine wanafanya kazi kwa malengo.

Akizungumzia juu ya uzinduzi wa mpango mkakati, Mkurugenzi Mtendaji wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia alielezea malengo ya taasisi kwa miaka ijayo ni kutazamia mbali VVU/ UKIMWI na kushughulika na magonjwa mengine yenye vitisho katika jamii, kulenga katika uhamasishaji wa rasilimali na kuchunguza ushirikiano wa pamoja na sekta binafsi ili kuendelea kutoa huduma zake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...