Na Agness Moshi- MAELEZO,

Ni takribani mwaka mmoja sasa tangu taarifa za kujengwa kwa Mradi wa Bomba la Mafuta litakaloanzia Hoima Nchini Uganda mpaka Tanzania kwenye bandari ya Tanga kuenea kwenye vyombo vya habari ,mitandao ya kijamii na kwa wakazi wa Mkoa wa Tanga ambao ndio wahusika wakuu kwenye mradi huu japo unajengwa kwa manufaa ya mataifa haya mawili kwa ujumla.

Mradi huu ni moja kati ya miradi mikubwa ambayo Nchi imeweza kutekeleza na utagharimu kiasi cha dola za Kimarekani Billioni 3.5 ambazo ni sawa na Tsh Trillioni 8 kwa fedha za kitanzania. Bomba hili linategemewa kuwa na urefu wa kilometa 1,445 likiwa na uwezo wa kusafirisha mapipa ya mafuta takribani 2,016,000 kwa siku na kutoa ajira zaidi ya 1,000 na vibarua zaidi ya 30,000.

Taarifa hizo zilianza kuwa rasmi, mnamo tarehe 14 marchi 2016 ambapo Makamu wa Rais wa kampuni ya Total Afrika Mashariki Bw.Javier Rielo alimhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kuanza kwa ujenzi wa Mradi huo.

Nyota njema ya Mradi huu ilianza kuonekana Aprili 24 ya mwaka jana, baada ya aliyekua Waziri wa Nishati na Madini Prof.Sospeter Muhongo kurejea Nchini kutoka Uganda, kuongea na waandishi wa habari kuhusu makubaliano yaliyofikiwa kwa mradi huo.

Bwana Muhongo alisema kuwa, kulikua na mjadala mkubwa wa kuchagua wapi Mradi huo ujengwe na wapinzani wakubwa kwa Tanzania walikua Kenya lakini kutokana na ubora wa bandari ya Tanga ukilinganisha na bandari nyingine Tanzania ilichaguliwa kunufaika na mradi huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...