MWEKA HAZINA wa miaka mingi wa Kilimanjaro Band, ambaye alijulikana kwa wapenzi wengi kutokana na kuwa mkata tiketi wa bendi wa miaka mingi sana, Francis Mnguto, maarufu kwa jina la Babu Francis amefariki leo alfajiri nyumbani kwake Ilala Flats Dar es Salaam. 
 
Kwa miezi kadhaa Babu Francis amekuwa akisumbuliwa na tatizo la figo. Taarifa kutoka kwa familia ni kuwa mazishi yatakuwa Dar es Salaam Jumatano 23 Agosti. Msiba upo nyumbani kwake Ilala Flats Dar es Salaam.

 
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...