BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imeridhishwa na idadi kubwa ya watii kutoka nchini China na kuelezea kuwa endapo kutakuwa na safari za ndege za moja kwa moja kutoka Tanzania kutasaidia kupunguza gharama za safari na pia kuchochea utalii.

Mwenyekiti wa Bodi ya TTB Jaji Mstaafu Thomas Mihayo aliwaambia waandishi wa habari jijini hapa juzi kuwa endapo kutakuwepo na ndege ya moja kwa moja kutoka Tanzania mpaka China, idadi kubwa ya watilii kutoka nchi hiyo itaongezeka na pia mataifa mengine, hivyo sekta ya utalii uchangia zaidi mapato ya serikali.

akizungumza mara baada ya kumaliza ziara ya kuwatembeza waandishi waandamizi wa habari kutoka nchini China katika hifadhi za Ngorongoro Crater na Manyara,Jaji Mihayo alisema vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini ni tunu kubwa kwa taifa na pia vinawaleta watalii kutoka sehemu mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii(TTB) Bi.Devota Mdachi(wanne kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja waandishi Waandamizi wa habari kutoka China walipotembelea hifadhi ya Ngorongoro Crater na Ziwa Manyara na kujionea fahari ya Tanzania. Lengo la ziara ya waandishi hao ni kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kwenda kuvitangaza kupitia makala na machapisho ili kuvutia wachina wengi kutembelea Tanzania.

“Ujio wa wanahabari hawa ni fursa kwetu kwani watakwenda kuwa mabalozi wazuri kwa kutoa machapisho na habari nchini kwao juu ya vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania,” alisema na kutoa wito kwa waandishi wa ndani kuunga mkono jitihada hizo.

Alisema waandishi hao kutoka China wameonyesha nia ya dhati ya kuvitangaza vivutio vyetu na hivyo kutokana na urafiki wa kihistoria uliopo kati ya China na Tanzania, zoezi hilo litakuwa la mafanikio makubwa.

Aliongezea kuwa China ni nchini yenye watu wengi Dunia hivyo kupitia waandishi hawa watakwenda kuwafikia wananchi wengi wa nchi hiyo kupitia makala na machapisho mbalimbali kuhusiana na vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania.
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof.Jumanne Maghembe(kushoto) akizungumza na waandishi waandamizi wa habari kutoka China mara baada ya kumaliza ziara yao ya kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro Crater na Ziwa Manyara. Lengo la ziara ya waandishi hao ni kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kwenda kuvitangaza kupitia makala na machapisho ili kuvutia wachina wengi kutembelea Tanzania.

“changamoto kubwa waliyoiona ni gharama ya usafari wa ndege ni kubwa kutokana na kutokuwepo kwa ndege za moja kwa moja,” alisema Jaji Mihayo na kuongezea kuwa usafiri wa anga utakapo imarishwa utachochea idadi kubwa ya watalii kutoka China. Alisema tayari Rais Magufuli alishaahidi kuleta ndege Kubwa itakayofanya safari ndefu hivyo itasaidia kupata soko la watalii kutoka china kuongezeka na itasaidia kuongeza mapato katika sekta ya utalii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...