Na Profesa Joseph Mbele

Tumo katika wiki ya mwisho ya kozi ya "African Literature," ambayo ni kwa kipindi hiki cha kiangazi. Kati ya vitabu ambavyo tumesoma ni Confession of the Lioness, riwaya ya Mia Couto wa Msumbiji. Couto ni mmoja wa waandishi maarufu kabisa Afrika na ulimwenguni, ambaye amepata tuzo za kimataifa kwa uandishi wake, ikiwamo tuzo ya Neustadt.

Mia Couto anaandika kwa ki-Reno. Ninasoma na kufundisha tafsiri za ki-Ingereza. Kwanza nilifundisha riwaya yake The Tuner of Silences hapa chuoni St. Olaf nikaipenda sana. Niliifundisha tena katika muhula mwingine. Kutokana na hilo, niliamua kufundisha riwaya yake nyingine. Ndipo nikachagua Confession of the Lioness, baada ya kusoma taarifa zake mtandaoni.
Riwaya hii inasimulia habari za eneo la kaskazini mwa Msumbiji, katika jamii ya wa-Makonde. Jamii inaishi kwa hofu na wasi wasi kutokana na kuwepo kwa simba ambao huzunguka na hushambulia watu na mifugo. Wasi wasi umechanganyika na imani za kishirikina kuhusu simba hao. Je, ni simba kweli, au ni simba wa kutengenezwa kiuchawi? Hilo ni moja ya maswali yanayosumbua jamii hii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...