* Niwakati mwingine tena Vodacom Tanzania imewaletea wateja wake na watanzania wote kwa ujumla  promosheni mpya kabambe kabisa inayojulikana kama Tusua Mapene. Promosheni hii itawawezesha wateja wetu na wananchi wote kwa wale ambao watajiunga na mtandao wetu kushiriki katika bahati nasibu na kujishindia vitita mbalimbali  mpaka kiasi cha shilingi milioni 150 ndani ya siku 150. 
Promosheni hii inampa mteja wa vodacom fursa ya kushiriki kupitia ujumbe mfupi wa maneno, huduma ya M-pesa au mitandao ya kijamii. 
*Vodacom itatoa mshindi mmoja wa Sh. 100M/-, washindi watano wa Sh. 20M/- na mshindi moja wa Sh. 15M/- KILA SIKU na mshindi wa mwisho wa promosheni(Grand draw) atajishindia kitita cha shilingi Million 150/- 
*Jinsi yakushiriki katika promosheni hii ni rahisi sana mteja anachotakiwa kufanya ni kutuma neno  “CHECK” au “VODA” kupitia ujumbe mfupi wa maneno kwenda namba 15544, kwa gharama ya shilingi 300 tu ikijumuisha kodi kwa kila ujumbe.
 Meneja huduma za Ziada na Tehama wa Vodacom Tanzania,Mathew Kampambe(kushoto) na Msimamizi wa michezo  ya kubahatisha nchini,Abdallah Hemed(kulia)wakimsikiliza Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Matina Nkurlu(katikati)alipokuwa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Promosheni mpya ya Tusua Mapene inayoendeshwa na kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam leo ambapo mkazi wa mkoa wa singida Munira Jumanne alijishindia Tsh. Laki 5/- Ili Mteja wa Vodacom aweze kushiriki kwenye promosheni hii anatakiwa kutuma neno  “CHECK” au “VODA” kwenda namba 15544, kwa gharama ya shilingi 300 tu.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Matina Nkurlu(kulia)akiongea kwa njia ya simu ya mkononi na mshindi  aliejishindia Tsh. Laki 5/- Munira Jumanne Mkazi wa mkoa wa Singida wakati wa Uzinduzi wa Promosheni mpya ya Tusua Mapene inayoendeshwa na kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo,Ili Mteja wa Vodacom aweze kushiriki kwenye promosheni hii anatakiwa kutuma neno  “CHECK” au “VODA” kwenda namba 15544, kwa gharama ya shilingi 300 tu.Anaeshuhudia kushoto ni Meneja huduma za Ziada na Tehama wa Vodacom Tanzania,Mathew Kampambe.
Meneja huduma za Ziada na Tehama wa Vodacom Tanzania,Mathew Kampambe(kushoto) na Msimamizi wa michezo  ya kubahatisha nchini,Abdallah Hemed(kulia)wakionyeshwa na  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Matina Nkurlu(katikati) namba ya simu ya mshindi  aliejishindia Tsh. Laki 5/- Munira Jumanne Mkazi wa Singida wakati wa Uzinduzi wa Promosheni mpya ya Tusua Mapene inayoendeshwa na kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam leo. Ili Mteja wa Vodacom aweze kushiriki kwenye promosheni hii anatakiwa kutuma neno  “CHECK” au “VODA” kwenda namba 15544, kwa gharama ya shilingi 300 tu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...