THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MKUTANO MKUU WA UCHAGUZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA NORTHAMPTON, UINGEREZA, KUFANYIKA JUMAMOSI AGOSTI 19, 2017


Ndugu wana Northampton kwa mujibu wa taratibu na kanuni tulizojiwekea na matarajio yetu ya muda mrefu, Kwa niaba ya kamati ndogo ya maandalizi naitisha Mkutano Mkuu na wa Uchaguzi wa Viongozi Wapya wa Jumuiya yetu ya Watanzania wote waishio Northampton na maeneo ya Wellingborough, Kattering na Corby (NORTHAMPTONSHIRE)  utakaofanyika siku ya Jumamosi tarehe 19/08/2017 katika ukumbi wa Norfolk Terrace, Semilong, Northampton NN2 6HS - Kuanzia saa kumi kamili jioni (4pm) mpaka saa mbili usiku (8.00pm).


Kamati ya maandalizi  inaomba ushirikiano wenu ili Kuepuka kupoteza muda siku ya mkutano, Tunaomba kila mjumbe mwenye ajenda ya ziada yeyote ambayo angependa iwepo katika kikao chetu basi asisite kunipatia siku nne kabla ya mkutano kwa njia ya Barua Pepe kwenda; suleimansalum160@yahoo.com au kwa kupiga simu ya Mkononi nambari 07963549935.
Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa  Tanzania Diaspora Community/Association in the United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland Ndugu Abraham Sangiwa, ambaye atatoa ufafanuzi wa jinsi Jumuiya zetu hapa Northampton zitakavoshirikiana na Jumuiya hii kuu katika malengo muhimu yanayotugusa wote Kama Watanzania tunaoishi Ughaibuni ili kupata ufumbuzi wenye nguvu zaidi kwa ushirikiano wetu.Tujitahidi kuzingatia muda siku hiyo.  
UMOJA NA NGUVU
Suleiman Salum
Mwenyekiti Jumuiya ya Watanzania Northampton