THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

UHURU NA RUTO WAIBUKA KIDEDEA UCHAGUZI MKUU WA KENYA

Uhuru Kenyatta hatimaye ametangazwa mshindi wa kiti cha Urais nchini Kenya, jambo ambalo limehitimisha siku kadhaa za sintofahamu kufuatia uchaguzi mkuu uliojaa ushindani mkubwa.
Rais mteule Uhuru alitangazwa mshindi kwa kujipatia jumla ya kura 8, 203,290  au asilimia 54.27 na Mwenyekiti wa Tume y Uchaguzi Wafura Chebukati wakati mshindani wake wa karibu  Raila Odinga wa  NASA akimfuatia kwa kura 6, 762, 224 ambazo ni asilimia 44.74% siku ya Ijumaa Agosti 11, ikiwa ni siku tatu baada ya kura kupigwa.
 "Naomba kumtangaza Uhuru Kenyatta kuwa Rais mteule na William Ruto Naibu Rais Mteule," alisema  Chebukati huku akishangiliwa na wafuasi wa washindi hao.
Uhuru alijizolea asilimia 25 ya kura katika majimbo 35 ambapo Raila alifanya hivyo katika majimbo 29.
Chebukati alisema jumla ya  Wakenya 15,073,662 walipiga kura ikiwa ni sawa na asilimia 71.91 ya waliojiandikisha.