THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

UJENZI WA MAEGESHO LINDI KITUNDA WAFIKIA HATUA NZURI

 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dk. Mussa Mgwatu (kulia)akimuonyesha mkandarasi wa kampuni inayojenga maegesho ya Lindi Kitunda Mhandisi Evans Martin eneo la maegesho ya kivuko wakati alipokua akikagua maendeleo ya ujenzi wa maegesho hayo mjini Lindi.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dk. Mussa Mgwatu (wa pili kulia) aliyenyoosha mkono, akimuonyeshea Meneja wa TEMESA Mkoa wa Lindi Mhandisi Greyson Maleko (wa kwanza kulia)  eneo patakapojengwa chumba cha  kupumzikia abiria wakati wakisubiria kivuko upande wa Kitunda. Dk. Mgwatu alikua Mkoani humo kukagua ujenzi wa maegesho ya Lindi Kitunda.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dk. Mussa Mgwatu akimsisitizia jambo Mkandarasi wa kampuni inayojenga maegesho ya Lindi Kitunda Mhandisi Evans Martin (wa kwanza kushoto) wakati alipokua akikagua maendeleo ya ujenzi wa maegesho hayo mkoani Lindi, nyuma yake ni Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA)   Mkoa wa Lindi  Mhandisi Hillary Msaki.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dk. Mussa Mgwatu kushoto Akimsikiliza Mhandisi Athaniel Kishebuka wakati alipotembelea banda la wakala huo katika maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi. Dk. Mgwatu yupo mjini Lindi kukagua maendeleo ya ujenzi wa maegesho ya Lindi Kitunda unaoendelea. PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA)