SHIRIKA
la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limekabidhi
vifaa vya radio kwa radio za jamii nne vyenye thamani ya mamilioni ya
shilingi. Unesco imesema kwamba utoaji wa vifaa hivyo umelenga kuongeza
usikivu wa mawimbi ya radio katika maeneo ya vijijini.
Shughuli
ya kukabidhiana imefanyika Agosti 17 mwaka huu. Akizungumza wakati
wakukabidhiana vifaa hivyo Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
Tanzania, Zulmira Rodrigues alisema kwamba UNESCO inatambua kazi nzuri
zinazofanywa na radio hizo za jamii za kuwafikia wananchi wengi zaidi. Mkuu
wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues
(kushoto) akizungumza jambo wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya radio
jamii iliyofanyika katika ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.
Aidha
alisema ni muhimu sana kwa radio hizo za jamii kujiangalia na kujitunza
zenyewe ili wasiingie katika matata na kuchapisha au kutangaza stori
baada ya kukamilika kwake. Alisema ipo haja kwa vyombo vya habari
kufanyakazi kwa mujibu wa taratibu zao na kuhakikisha kwamba
hawachapishi habari ambazo zinahatarisha uwapo wa uandishi unaozingatia
maadili. Meneja wa radio ya Jamii ya Baloha FM, Samada Maduhu
aliishukuru UNESCO kwa kusaidia kituo chake na kwamba wanatarajia
kufikia wilaya tano. Meneja
wa radio ya Jamii ya Baloha FM ya Kahama, Samada Maduhu, akitoa neno la
shukrani kwa ofisi za Unesco wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya
vifaa hivyo yaliyofanyika katika ofisi za Shirika hilo jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Ofisa mtaalamu wa Mawasiliano Unesco, Nancy Kaizilege
Angulo.
Alishukuru
UNESCO kwa kuwawezesha kufika katika wilaya tano na kwamba kwa msaada
huo wataokoa shilingi laki saba kwa mwezi kuazima transmita. “Radio yetu
inawafikia watu 500,000 lakini kwa kupatiwa hivi vifaa tutaweza kufikia
watu milioni 1 katika wilaya zaidi ya tano za Kahama, Shinyanga
Vijijini, Nyang’wale na Mbogwe mkoani Geita na pia Nzega na Uyui mkoani
Tabora ,” alisema meneja huyo . Kwa mujibu wa Maduhu, kama wasingelipata
transmita hiyo wangelikuwa wanatumia sh milioni 8.4 kwa mwaka. Ofisa
Utawala na Rasilimali Watu wa Radio Jamii ya Pangani FM, Rehema
Kilapilo akitoa shukrani kwa uongozi wa Unesco wakati wa hafla ya
makabidhiano ya vifaa vya redio iliyofanyika katika ofisi za Unesco
jijini Dar es Salaam.
Kwa
upande wake, Ayubu Kalufya wa radio ya jamii Uvinza alisema kwamba
kituo chake kilikuwa kinakodisha transmita kwash laki tano na kufanya
kwa mwaka mzima kutumia sh milioni 6. Alisema kwa kupata vifaa hivyo
walikuwa wanaachama na ukodishaji huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...