Na Chalila Kibuda,GlobuyaLindi

Katika kukabiliana na changamoto za madhara ya ajali za pikipiki yanayosababishwa na madereva kutovaa kofia ngumu (helmet), Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imebuni teknolojia ya kukabiliana na hilo.

Mwalimu wa fani ya elektroniki kutoka VETA Kipawa, AnethMganga, amebuni mfumo wa kielektroniki unaozuia pikipiki kuwaka mpaka dereva awe amevaa kofia ngumu (helmet).

Akizungumza katika viwanja vya maonesho ya Nanenane Ngongo, mkoani Lindi, mwalimu Aneth amesema mfumo huo ukianza kutumika na madereva wa pikipiki utapunguza madhara endapo kunatokea ajali kwa kuwa bila ya kuvaa kofia ngumu pikipiki haiwezi kuwaka na hata ukiwa katika mwendo ikitokea ukavua kofiangumu pikipiki itazimika.

Aidha, katika usalama barabarani inasaidia kuzuia wizi wa pikipiki kwani mwizi hatoweza kuiwasha bila kofiangumu ambayo imeunganishwa kieletroniki.

Aneth amesema anaendelea kufanya utafiti nakuboresha zaidi ubunifu huo, lakini ameomba serikali na wadau mbalimbali kuunga mkono ili uweze kuenea, kukubalikana kutumika na waendesha pikipiki katika maeneo mbalimbali nchini.

Mkuu wa wilaya ya Newala, Aziza Mangosongo, akitembelea banda la VETA katika maonesho ya Kilimo 2017 yanayoendelea mkoani Lindi katika viwanja  vya Ngongo ambapo alipongeza VETA kwa kuweka fursa nyingi za mafunzo ya ujuzi kwa makundi mbalimbali ya wananchi. Aliahidi kushirikiana na VETA ilikuwa wezesha wananchi wilaya ni kwake kunufaika pia na fursa mbalimbali za mafunzo ya ufundi stadi. 
Wanafunzi wa shule ya sekondari Medi ya mkoani Mtwara wakipata maelekezo juu ya aina ya mafunzo yanayotolewa katika vyuo vya ufundi Stadi walipotembelea banda la VETA katika Maonyesho ya kilimo ya Nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
.Mwalimu wa Elektroniki wa Veta Kipawa, Aneth Mganga akiwapa maelezo wananchi waliotembelea banda la VETA Pikipiki inayoendeshwa ni lazima dereva awe amevaa kofiangumu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...