Na Chalila Kibuda, Lindi

Kwa mara nyingine tena Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imepata ushindi wa kwanza kwenye kundi la Taasisi za Utafiti na Mafunzo katika maonesho ya Wakulima Nanenane, 2017 yaliyokuwa yakifanyika kitaifa kwenye uwanja wa Ngongo mkoani Lindi.

Baada ya kutangazwa mshindi katika sherehe za ufungaji rasmi wa Maonesho, VETA imekabidhiwa kombe na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika shughuli za ufungaji wa maonesho hayo zilizofanyika leo 8 Agosti, 2017. 

VETA ilifuatiwa na Chuo cha Maji katika nafasi ya pili na Chuo cha Uhasibu Arusha ambacho kilishika nafasi ya tatu katika kundi hilo. Kaulimbiu ya maonesho hayo ilikuwa, "Zalisha kwa Tija Mazao na Bidhaa za Kilimo, Ufugaji na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati." 

Katika maonesho hayo, VETA ililenga kutoa taarifa na kuhamasisha wananchi kutumia fursa mbalimbali za mafunzo ya ufundi stadi ili kuboresha shughuli za kilimo, ufugaji na uvuvi, hivyo kuzalisha kwa tija. 

Vilevile VETA ilionesha ubunifu wa teknolojia bora na rahisi katika kilimo, mifugo na uvuvi na kwa ajili ya kuboresha maisha ya jamii ya wananchi wa kijijini. 

Mfano wa ubunifu na teknolojia ni pamoja na mashine za kufukuza ndege waharibifu wa mazao mashambani, vifaa vya kumwagilia, ujenzi wa nyumba kwa gharama nafuu, mashine za kisasa za usanifu wa nguo, jiko la kisasa linalotumia mafuta ya taa na nyinginezo. 
Mkuu wa Chuo cha VETA Lindi akipeana mkono na Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu baada ya VETA kuchukua kikombe cha mshindi wa kwanza wa Taasisi Mafunzo ya Ufundi Stadi katika kilele cha maonesho ya Kitaifa ya Nanenane katika viwanja Ngongo mkoani Lindi.
Watendaji na Veta wakishangalia baada ya kupata kikombe cha mshindi wa kwanza wa Taasisi Mafunzo ya Ufundi Stadi katika kilele cha maonesho ya Kitaifa ya Nanenane katika viwanja Ngongo mkoani Lindi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...