Timu zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom tanzania bara zimekabidhiwa vifaa mbalimbali na mdhamini mkuu wa ligi hiyo Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, vifaa hivyo vilivyokabidhiwa kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo vina thamani ya zaidi ya shilingi milioni 500/=

Akikabidhi vifaa hivyo jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Masoko na Usambazaji wa kampuni hiyo, Hisham Hendi, alisema kuwa  kwa mara nyingine tena katika kuhakikisha ligi ya soka nchini inaenda vizuri Vodacom inakabidhi  vifaa mbalimbali vya ligi ambavyo ni jezi mbalimbali, viatu vya mazoezi na mechi, soksi, vilinda ugoko, nguo za mazoezi, nguo za kawaida, gloves, mabegi ya kusafiria, nguo za marefa, bendera, substitution boards  na vifaa vingine vingi vinavyohitajika. “Tunajisikia furaha  kukabidhi vifaa hivi siku ya leo tukiwa tunatekeleza  matakwa ya mkataba wa udhamini, ni imani yetu kwamba timu zitakazoshiriki ligi zimejiandaa vya kutosha kwa msimu mpya wa ligi  wa 2017/2018”Alisema Hendi.

Hendi alisema Vodacom inaendelea kudhamini ligi kuu kwa sababu soka ni mchezo unaopendwa sana hapa nyumbani ukiwa na washabiki wengi hivyo inapenda kuona wananchi ambao baadhi yao ni wateja wake wanapata burudani ya mchezo waupendao pia siku zote inaamini kuwa michezo ni ajira kubwa duniani kote, ikiendelezwa inaweza kubadilisha maisha ya watu wengi na taifa kunufaika kwa mapato makubwa ya kodi kutoka katika sekta hii.
Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Masoko na Usambazaji wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi(kulia) akimshuhudia Mwakilishi wa timu ya Yanga ambaye ni Afisa habari wa timu ya Simba, Haji Manara(kushoto) baada ya timu hiyo kukosa mwakilishi akimtania mmoja wa vijana aliyeitambulisha jezi ya Yanga itakayotumika katika msimu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2017/2018 wakati wa hafla iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ya  kukabidhi vifaa kwa timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura akipokea keki toka kwa Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Masoko na Usambazaji wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi(kulia)kuashiria Uzinduzi wa msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,wakati wa hafla iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ya  kukabidhi vifaa kwa timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Masoko na Usambazaji wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi(kulia)akimpongeza mmoja wa vijana aliyeitambulisha jezi ya Azam FC wakati wa hafla iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ya  kukabidhi vifaa kwa timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo jana jijini Dar es Salaam,Kutoka kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura na Mwakilishi wa Timu hiyo, Jafari Maganga.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura(kushoto)akiwashuhudia mwakilishi wa timu ya  Simba Afisa habari wa timu hiyo, Haji Manara(watatu kushoto)pamoja na Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Masoko na Usambazaji wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi(kulia)wakiwapongeza vijana walioitambulisha jezi ya nyumbani na ugenini ya timu hiyo wakati wa hafla iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ya  kukabidhi vifaa kwa timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo jana jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...