NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

WAFANYAKAZI wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kupitia chama chao cha TUICO, wamemponegza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kwa mchango wake mkubwa katika kuendeleza sekta ya umeme nchini ambapo kampeni yake ya “KA..TA” imekuwa na mafanikio makubwa ambapo wale wadaiwa sugu sasa wanalipa madeni yao.

Akitoa salamu za pongezi kwa Rais leo Agosti 10, 2017, kwenye makao makuu ya TANESCO Ubungo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Majadiliano ya TUICO, tawi la TANESCO, Bw.Hassan J.M Athumani, alisema, Mhe. Rais Magufuli, amewezesha TANESCO kukusanya madeni yake hata maeneo ambayo ilikuwa vigumu sana kulipa madeni.

“Wakati kampeni ya KA..TA ilipoanza mwezi Machi mwaka huu wa 2017, deni lilikuwa shilingi bilioni 275, kati ya hizo, taasisi za serikali pamoja na Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), zilikuwa zinadaiwa shilingi Bilioni 180 wakati taasisi binafsi, zilikuwa zinadaiwa shilingi Bilioni 95.

Bw. Athumani alisema ZECO pekee tayari wamelipa shilingi bilioni 18, wakati taasisi za serikali yakiwemo majeshi wamelipa deni shilingi Bilioni 18 pia, huku wadaiwa binafsi (private) wamelipa shilingi bilioni 5 na hivyo kufanya deni lililolipwa kufikia Julai 2017, kufikia shilingi bilioni 41.

“Kampeni hii ya rais ya KA..TA, imewezesha TANESCO sasa kukusanya bili za umeme hadi asilimia 104 kwa mwezi kutoka asilimia 90 kwa mwezi kabla ya kuanza kwa kampeni hii.” Alifafanua Mkuu wa Fedha wa TANESCO Bw.Philidon Siyame


Mwenyekiti wa Kamati ya Majadiliano ya TUICO, Tawi la TANESCO, Bw. Hassan JM. Athumani, akizungumza wakati wa kutoa tamko la Wafanyakazi wa TANESCO kupitia chama chao cha TUICO kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kufuatia kampeni aliyoianzisha ya ukusanyaji wa madeni ya bili za umeme ijulikanayo kama "KA..TA". Tamko hilo alilitoa mbele ya wajumbe wa kamati kwenye ukumbi wa mikutano wa TANESCO makao makuu jijini Dar es Salaam, leo Agosti 10, 2017.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Majadiliano ya TUICO tawi la TANESCO, kutoka kushoto, Bw.Ahmed Mwinyi, ayewakilisha wafanyakazi upande wa uzalishaji umeme kwa njia ya mafuta (Themo Generation), Bw.Felix Lyimo, anayewakilisha wafanyakazi kutoak Kanda ya Dar es Salaam na Pwani na Bi.Asha Mtola, anayewakilisha wafanyakazi wanawake wa Shirika hilo wakisikiliza wakati tamko hilo likitolewa na Mwenyekiti wao. .
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt.Tito Mwinuka, (wapili kushoto), Naibu Mkurugenzi Mtendaji (uwekezaji), Mhandisi Khalid James, (wakwaza kushoto) na baadhi ya wajumbe wa TUICO, wakinakili yaliyokuwa yakisemwa na Mwneyekiti wa TUICO Bw. Athumani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...