Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
WAFANYAKAZI watano wa zamani wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na msambazaji kutoka kampuni ya M/S Young Dong Electronic Co. Ltd, wamepandishwa katika kizimbani cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za uhujumu uchumi

Washtakiwa hao ambao wanadaiwa pia kuisabishia Serikali hasara ya M.275 wamefikishwa mahakamani hapo na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, TAKUKURU.

Mwendesha mashtaka, wakili wa Serikali Mkuu Vitalis Peter amewataja watuhumiw hao kuwa ni, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Robert Shemhilu, Ofisa Ugavi, Harun Mattambo, Mkurugenzi wa Fedha, Lusekelo Kasanga, Mwanasheria wao, Godson Makia pamoja na msambazaji Martin Simba.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka mawili yanayowakabili ya uhujumu uchumi na matumizi mabaya ya madaraka na kusababisha hasara mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Imedaiwa, Desemba 2011 katika ofisi za Tanesco Ubungo, washtakiwa wakiwa waajiriwa wa shirika hilo, walitumia madaraka yao vibaya kwa kufanikisha malipo kwa msambazaji Martin Simba bila ya kufanya uhakiki.

Imedaiwa kuwa washtakiwa walifanya hivyo kinyume na kifungu cha 35 cha Sheria ya Manunuzi ya Umma namba 21 ya 2014 kitendo ambacho kilisababisha msambazaji huyo kupata faida.

Wakili Vitalis aliendelea kudai kuwa kati ya Januari na Desemba, mwaka 2011 katika ofisi hizo za Tanesco, washtakiwa hao wote waliisababishia Serikali hasara ya Sh 275,040,000.

Hata hivyo, washtakiwa wamekana tuhuma hizo baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka DPP kuwasilisha Cheti maalum kilichoiruhusu Mahakama kuisikiliza kesi hiyo.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.
Hakimu Simba aliwataka washtakiwa hao kuwa na wadhamini wawili ambapo kila mmoja alitakiwa kuweka dhamana ya M.40.

Aidha,mahakama imeamuru mmoja kati ya washtakiwa hao awasilishe hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 24 mwaka huu itakapokuja kwa ajili kusomewa maelezo ya awali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...