THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

WAFUGAJI LONGIDO WAANZA KUNUFAIKA NA UJENZI WA SOKO LA KISASA LA MIFUGO

 

Benny Mwaipaja, WFM, LONGIDO-ARUSHA.

WAFUGAJI wilayani Longido Mkoani Arusha wameanza kunufaika na ujenzi wa soko la kisasa la mifugo linalojengwa na Serikali katika kijiji cha Worendeke kata ya Kimokouwa, kupitia mkopo wa fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB.

Baadhi ya wafugaji wamesema kuwa Soko hilo linalojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 650, limewaondolea adha kubwa waliyokuwa wakiipata walipokuwa wakiuza mifugo yao nchini Kenya kutokana na gharama kubwa ya kusafirisha mifugo kwenda huko pamoja na kulipa kodi na ushuru mbalimbali.

Wamesema kuwa kujengwa kwa somo hilo ni mkombozi mkubwa kwao na kwamba hali hiyo itasisimua uchumi wao kwa kuwa wafanyabiashara wa ndani na kutoka Kenya wamekuwa wakiwafuata kwenye soko hilo kununua mifugo yao hatua inayowafanya wapate faida kubwa.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Longido, Bw. Toba Nguvila, amesema kuwa soko hilo ambalo ujenzi wa miundombinu yake umekamilika kwa asilimia 85 limeanza kuiingiza Serikali mapato yake ambapo kwa wastani Halmashauri ya wilaya inakusanya wastani wa shilingi milioni 1 kwa siku.

“Asilimia 95 ya wakazi wa wilaya yetu ni wafugaji wa kimaasai ambao kwa kipindi kirefu wameteseka kusafirisha mifugo yao kwenda Kenya na kutopata faida kutokana na gharama kubwa ya kusafirisha, kupitisha mifugo kwenye maeneo ya watu hivyo kulazimika kulipa ushuru, halikadhalika kulipia tozo mbalimbali wakati wakisubiri kuuza mifugo yao” alieleza Bw. Nguvila .

Katibu Tawala wa Wilaya ya Longido mkoani Arusha, Bw. Toba Nguvila (kushoto), akimweleza jambo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro (katikati) kabla ya kutembelea Soko la Kisasa Mifugo linalojengwa katika kijiji cha Worendeke, kata ya Kimokouwa, wilayani Longido, mkoani Arusha, linalojengwa kutokana na mkopo wenye masharti nafuu wa sh. Milioni 650 kutoka Benki hiyo. Kulia ni Afisa anayeshughulikia Dawati la Beni ya Maendeleo ya Afrika-AfDB kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Said Nyenge. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro akisikiliza maelezo ya mradi wa ujenzi wa Soko la Kisasa la Mifugo katika kijiji cha Worendeke, kata ya Kimokouwa, wilayani Longido mkoani Arusha, unaogharimu shilingi milioni  650, ikiwa ni mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki hiyo. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro, akisisitiza jambo baada ya kusikiliza maelezo ya mradi huo wa Soko la Kisasa la Mifugo linalojengwa katika kijiji cha Worendeke, kata ya Kimokouwa wilayani Longido mkoani Arusha. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro (wapili kulia) akimweleza jambo Katibu Tawala wa wilaya ya Longido mkoani Arusha, Bw. Toba Nguvila, wakati Mkurugenzi huyo alipotembelea na kukagua ujenzi wa Soko la Kisasa la Mifugo, linalojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 650 kupitia mkopo nafuu wa Benki hiyo kwa Serikali ya Tanzania. 
Baadhi ya wafugaji wa kijiji cha Worendeke, kata ya Kimokouwa, wilayani Longido mkoani Arusha, wanaonufaika na uwepo wa soko hilo ambapo wameanza kuuza mifugo yao kwa faida kubwa badala ya kupeleka mifugo yao nchi jirani ya Kenya ambako walikuwa wakipata adha kubwa na faida ndogo kutokana na gharama kubwa walizokuwa wakitumia kufikisha mifugo yao nchini humo. (Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango) .