Na Mwamvua Mwinyi,Pwani 

JESHI la Polisi Mkoani Pwani ,linamshikilia mfanyabiashara anaedaiwa kuwasafirisha wahamiaji haramu 72 raia kutoka nchini Ethiopia,Rajabu Hitaji (30)mkazi wa Vigwaza ,Bagamoyo . Aidha jeshi hilo linawashikilia pia wahamiaji haramu hao kwa kosa la kuingia nchini bila kibali . 

Akitolea ufafanuzi juu ya tukio hilo ,kamanda wa Polisi mkoani Pwani(ACP) Jonathan Shanna ,alisema uchunguzi unaendelea na watafikishwa ofisi za uhamiaji kwa hatua nyingine stahiki. 

Alieleza ,mtuhumiwa Hitaji ambae ni mfanyabiashara alikamatwa jana, saa 3.30 asubuhi huko maeneo ya pori la ranchi ya Taifa Narco ,Vigwaza wilaya ya kipolisi Chalinze . 

“Kufuatia msako mkali ulioendeshwa na makachero wetu baada ya kupata taarifa juu ya uwepo wa raia walioingia nchini pasipo kufuata taratibu za uhamiaji na raia hao baada ya kugundua kuna gari la polisi linawafuatilia “
“Waliingia kwenye hifadhi hiyo kwa lengo la kujificha lakini askari wetu waliweza kubaini mahali walipo kufuatia msako mkali uliokuwa ukiendeshwa katika ranchi hiyo ” alisema kamanda Shanna . 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...