Na Mwamvua Mwinyi, Pwani.
JESHI la Polisi Mkoani Pwani, linamshikilia mfanyabiashara, Rajabu Hitaji (30) mkazi wa Vigwaza, Bagamoyo anaedaiwa kuwasafirisha wahamiaji haramu 72 raia kutoka nchini Ethiopia.

Aidha jeshi hilo linawashikilia pia wahamiaji haramu hao kwa kosa la kuingia nchini bila kibali .

Akitolea ufafanuzi juu ya tukio hilo ,kamanda wa Polisi mkoani Pwani(ACP) Jonathan Shanna, alisema uchunguzi unaendelea na watafikishwa ofisi za uhamiaji kwa hatua nyingine stahiki. Alieleza ,mtuhumiwa Hitaji alikamatwa majira ya saa 3.30 asubuhi huko maeneo ya pori la ranchi ya Taifa Narco ,Vigwaza wilaya ya kipolisi Chalinze.

"Kufuatia msako mkali ulioendeshwa na makachero wetu baada ya kupata taarifa juu ya uwepo wa raia walioingia nchini pasipo kufuata taratibu za uhamiaji na raia hao baada ya kugundua kuna gari la polisi linawafuatilia "

"Waliingia kwenye hifadhi hiyo kwa lengo la kujificha lakini askari wetu waliweza kubaini mahali walipo kufuatia msako mkali uliokuwa ukiendeshwa katika ranchi hiyo " alisema kamanda Shanna .

Alisema askari hao walifanikiwa kuwakamata kundi la kwanza la wahamiaji haramu 63 wakiwa mahali ambapo gari halifiki.

Kamanda Shanna ,alieleza kwamba, licha ya kukamatwa kundi hilo askari waliendelea na msako na kufanikiwa kukamata kundi jingine la wahamiaji haramu Tisa, waliokuwa wakitafuta njia ya kutoroka katika ranchi ya taifa ya Narco .

Wakati huo huo, MTU mmoja na watoto wawili wamefariki dunia baada ya mtumbwi waliokuwa wakitumia kuvuka mto Ruvu kuzama.

Mtumbwi huo walikuwa wakiutumia kutoka upande wa Vigwaza kwenda upande wa Mlandizi katika mto huo wilaya ya kipolisi Chalinze Mkoani Pwani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hawa ni binadamu watafuta maisha wasindikizwe wanakotaka kwenda

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...