THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

WAKUU WA WILAYA WAAGIZWA KUSIMAMIA UHAKIKI WA IDADI YA WAKULIMA WA TUMBAKU NA UWEZO WAO WA KULIMA ZAO HILO.

Na Tiganya Vincent-Tabora


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewaagiza Wakuu wa Wilaya kusimamia zoezi la kuhakiki idadi ya wakulima wa tumbaku na ukubwa mashamba ambayo wanaweza kulima kwa ajili ya kuweka mipango mizuri ya uagizaji wa pembejeo kulingana na mahitaji halisi.

Mhe. Majaliwa alitoa kauli hiyo jana mjini Tabora wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya siku nne mkoani hapo kuhimiza shughuli mbalimbali za maendeleo na vile vile kufuatilia zao la tumbaku.

Alisema kuwa lengo kutaka kuboresha uzalishaji wa zao hilo na kuweka mazingira ambayo mkulima hataendelea kunyonywa na baadhi watu ambao hawalimi tumbaku lakini ikifika wakati wa uuzaji wanajifanya nao ni wakulima wa tumbaku.

Waziri Mkuu aliongeza kuwa hatua hiyo pia itasaidia wataalamu wa eneo husika kuweza kujua kwa haraka mahitaji ya wakulima wa zao la tumbaku katika eneo lake na hivyo kuwasaidia ili waweze kuzalisha kwa wingi na tumbaku iliyo katika kiwango bora

Aidha Mhe. Majaliwa alisisitiza kuwa msimamo wa Serikali ni kuwa kila mkulima atauza tumbaku yake kupitia Chama cha Msingi na atapaswa awe amesajiliwa na Chama kilichopo katika eneo lake na sio vinginevyo.

Waziri Mkuu alisema kinyume cha hapo mtu yoyote awe Mwanasiasa au mtumishi wa umma atakayekamatwa anajihusisha na ununuzi wa tumbaku au uuzaji wa pembejeo za kilimo kinyume na maelekezo ya Serikali atakamatwa na hatua kali dhidi yake zitachukuliwa.

Mhe. Majaliwa aliziaagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama kuanzia ngazi ya Mkoa hadi Kijiji kukamata watu wote bila kuwaonea huruma wale wananunua tumbaku kwa njia ya vishada na wale wanaojihusisha na uuzaji wa mbolea kwa wakulima bila kuwa na vibali.