THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

WANAOVAMIA MAENEO, UJENZI HOLELA MANISPAA YA DODOMA SIKU ZAO ZINAHESABIKA

 MKURUGENZI wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi ametoa wito kwa wakazi wa Manispaa hiyo kuacha mara moja uvamizi wa maeneo ya wazi na yaliyotengwa kwa ajili ya hifadhi za misitu ambapo watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Aidha amewataka wanaojenga nyumba za makazi au za biashara katika maeneo yasiyo rasmi na ambayo hayakupimwa kusitisha shughuli za ujenzi na kubomoa majengo hayo kwa hiyari yao vinginevyo Halmashauri ya Manispaa itayabomoa.

Alisema hayo jana wakati akizungumza wa wamiliki wa nyumba za kupanga na Maofisa Watendaji wa Kata wa Manispaa ya Dodoma katika ukumbi wa Dodoma Sekondari, ambapo alisema kujenga katika maeneo yasiyopimwa ni kinyume na sheria na Manispaa ya Dodoma imejipanga kusimamia hilo kikamilifu.

Alisema Manispaa ya Dodoma imejipanga kuanza upimaji wa viwanja kwa kasi ili kuwawezesha wananchi  hususan wakazi wa Dodoma kujenga kwa kuzingatia sheria za Mipango Miji na kwamba upimaji huo utaenda sambamba na utoaji wa vibali vya ujenzi katika kipindi kisichozi siku saba kwa mmiliki wa kiwanja.

Kwa upande wa wamiliki wa nyumba za kupanga, aliwataka kuungana na kuwa na umoja na uongozi wao ili kuepukana na madalali ambao baadhi yao sio waaminifu, huku akiwapa changamoto ya kujenga nyumba zaidi za makazi na kuziimarisha zilizopo huku akiwajulisha kuwa, hivi karibuni watumishi  wa Serikali zaidi ya 2,000 wanatarajiwa kuhamia Mjini Dodoma ikiwa ni awamu ya pili ya Serikali kuhamia Dodoma hivyo mahitaji ya nyumba za kuishi yatakuwa makubwa.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi akizungumza na wamiliki wa nyumba za kupanga Manispaa ya Dodoma (hawapo pichani) wakati wa mkutano uliowakutanisha wadau hao na Mkurugenzi huyo jana Katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Dodoma. 

Baadhi ya wamiliki wa nyumba za kupanga katika Manispaa ya Dodoma wakimsikiliza Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (hayupo pichani) wakati wa mkutano uliowakutanisha wadau hao na Mkurugenzi huyo jana Katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Dodoma.  PICHA NA RAMDHANI JUMA.