THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

WANASAYANSI 200 KUONESHA KAZI ZAO JIJINI DAR

Mkurugenzi na muanzilishi wa Taasisi ya Young Scientist Tanzania(YST), Gozibert Kamugisha akizungumza na Waandiishi wa Habari juu ya Maonesho ya Wanasayansi Chipukizi yanayotaraji kuanza Agosti 8 mpaka 9 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es salaam. kulia ni Mkurugenzi wa Bg Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya Royal Dutch Shell, Marc den Hartag

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Maonesho ya elimu ya Sayansi kwa wanafunzi wa Sekondari maarufu kwa jina la 'Young Scientist' yanataraaji kuanza agosti 8 hadi 9 mwaka huu katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Taasisi ya Young Scientist Tanzania(YST),  Dr Gozibert Kamugisha amesema onesho hili la aina yake na litaonyesha kazi za kisayansi na ugunduzi kutoka kwa wanafunzi wa Sekondari 200 na walimu 100 kutoka mikoa yote Tanzania.

“kwa siku mbili za onesho wanasayansi Chipukizi wataonesha kazi zao katika Nyanja mbalimbali za Sayansi kama vile kemia, fizikia, hesabu, Bailojia, ekolojia, Sayansi ya Jamii na Teknonojia. hivyo kazi nyigi zitakazooneshwa zimejikita katika kutoa njia za kukabiliana na matatizo ya afya, Kilimo na usalama wa matatizo ya kijamii zaidi”Amesema Kamugisha.

Amesema Onesho hilo limewezeshwa na udhamini endelevu wa BG Tanzaniaa ambayo ni kampuni tanzu ya Royal Dutch ShellPlc na wadhamini wengine. Ametaja kuwa Wanasayansi Chipukizi watakaonesha kazi nzuri watazawadiwa pesa Taslimu ,Vikombe ,Medali na Vifaa vya Maabara.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Shell Afrikaa ya Mashariki na Bg Tanzaniaa, Marc den Hartog amesema kuwa wao kama Shell wanaona fahari kubwa kuwa mdhamini wa mashindno hayo kwa kwa kufanya hivyo ndivyo wataweza kupata wanasayansi wa baadae ambao wataweza kusaidia katika uchumi wa Viwanda na sekta ya gesi na mafuta .
Mkurugenzi wa Shell Afrika Mashariki na Bg Tanzania, Marc Den Hartog akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya namna kampuni yake inavyodhamini Maonesho hayo yenye manufa kwa kizazi cha kuwaandaa magwiji wa Sayansi nchini. 
Muasisi na Mkurugenzi wa ushauri wa Masuaala ya Kisayansi, Joseph Clowry akizuungumza mafanikio ya tasisi hiyo ndani ya miaka sita tangu ianze kuendesha maonesho hayo.
Waandishi wa habari wakiendelea na mkutano huo katika Hotel ya Golden Tulip iliyopo katikati ya jiji.