THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Washiriki kutoka Tanzania wa “Young African Leaders Initiative (YALI) 2017” watembelea Ubalozi wa Tanzania, Washington, D.C

Tarehe 2, Agosti 2017) Washiriki 42 wa Mandela Washington Fellowship 2017 kutoka Tanzania waliofika mwezi Juni, 2017, walitembelea Ubalozi wa Tanzania, Washington, D.C. na kukutana na Balozi Wilson M. Masilingi. 

YALI, ni programu iliyoanzishwa na Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama kuwasaidia vijana wa Afrika kutembelea Vyuo vikuu vya Marekani kujifunza, kwa ufadhili wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani (U.S. Department of State). Baada ya kumaliza mafunzo katika vyuo mbalimbali Watanzania hao walitembelea Washington, D.C. kupokea vyeti na kutembelea Ubalozi wa Tanzania.

Balozi Masilingi aliwaasa kuwa wazalendo, kupendana na kuwa waadilifu katika kuendeleza uchumi wa nchi yetu kwa kuanzisha na kukuza biashara. Aliwashauri pia kushirikiana na Ubalozi na Diaspora ya Watanzania waliopo Marekani, kukuza sekta ya utalii, biashara, elimu na ujenzi wa viwanda.
Balozi Tanzania nchini Marekani, Wilson M. Masilingi akizungumza na Washiriki wa YALI, Mandela Wahington Fellows. (kulia) Afisa wa Ubalozi, Dismas Assenga.
Yali Mandela Washington Fellows 2017 wakiongea na Mhe. Balozi.
Balozi Wilson M. Masilingi akiwa na washiriki wa YALI Mandela Washington Fellows, 2017.