MTU mmoja na watoto wawili wamefariki dunia baada ya mtumbwi waliokuwa wakitumia kuvuka mto Ruvu  kuzama Mkoani Pwani. 

Mtumbwi huo walikuwa wakiutumia kutoka upande wa Vigwaza kwenda upande wa Mlandizi katika mto huo wilaya ya kipolisi Chalinze Mkoani Pwani.

Kamanda Shanna amesema, tukio hilo limetokea majira ya saa kumi alfariji usiku wa kuamkia Agosti 6 mwaka huu.

Aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni Sikuzani Mussa (41) ambae mwili wake bado haujapatikana na jitihada za kuutafuta zinaendelea.

Kamanda Shanna, alisema watoto waliopoteza maisha kwenye tukio hilo ni Nusurat Haji mwenye miezi minne na Fesali Hamza mwenye mwaka mmoja.

Aidha katika tukio hilo watu wawili waliweza kuokolewa wakiwa hai ambao ni Zuwena Ramadhani (29)na Tero Mziray (20).

"Dereva wa mtumbwi huo haijajulikana alipo na inaaminika ya kwamba yeye hajafa maji.''

Kamanda Shanna, alieleza chanzo cha mtumbwi huo kuzama maji bado kinachunguzwa na miili ya marehemu imeshafanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu zao kwa ajili ya mazishi .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...