THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MICHUZI TV: WAZIRI LWENGE ATEMBELEA MIRADI YA MAJI YA DAWASA, DAR NA PWANIKazi zinazo fanyika chini ya Mradi huu ni pamoja na ujenzi wa matenki tisa (9) ya kusambaza na kuhifadhi maji yenye ukubwa wa kuhifadhi lita milioni 3.0 hadi milioni 6.0, ujenzi wa vituo vinne (4) vya kusukuma maji, ununuzi na ufungaji wa Pampu kubwa za kusukuma maji 16, ununuzi wa transfoma na ufungaji njia za Umeme wa msongo mkubwa, ununuzi na ulazaji wa mabomba makubwa ya ugawaji maji na ulazaji maji wa mabomba ya usambazaji maji mtaani yatakayokuwa na urefu wa jumla ya kilometa zipatazo 477.  

Maeneo yatakayo nufaika na mradi huu ni pamoja na Salasala, Bunju, Wazo, Makongo, Changanyikeni, Bagamoyo, Mpiji, Zinga, Kitope, Ukuni, Kerenge, Buma, Mataya na ukanda maalum wa EPZA ambayo ni maeneo yanayo hudumiwa na mtambo wa Ruvu chini. Ambayo ni maeneo mengine yatakayo nufaika na mradi huu ni yale yaliyopo kati ya Mbezi luisi na kiluvya, ambayo ni Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Msakuzi, Makabe, Malamba mawili na Msigani. Maeneo haya huhudumiwa na mtambo wa ruvu juu ambao ulizinduliwa na mh,Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Juni 21,2017.

Lengo la mradi huu ni pamoja na kuhakikisha kuwa wananchi wa kawaida , wenye viwanda na biashara katika eneo lote la mradi wanapata huduma bora za Maji hasa baada ya maji kuongezeka kufuatia kukamilika kwa upanuzi wa mitambo ya maji ya Ruvu juu na Ruvu chini. Lengo lengine ni kuweka mitandao ya maji katika maeneo mengine ambayo hayakuwa na mtandao rasmi wa maji, kwa kufanya hivi mradi utawezesha maji yagawanywe kwa urahisi na uwiano zaidi.

Ili kudhibiti upotevu wa maji, mita maalum zitafungwa katika maeneo ya kupokea maji na katika matoleo ili kujuwa kiasi kamili cha maji kilicho ingia katika eneo husika na kiasi cha maji  moja kwa moja ofisi za (DAWASCO) ambapo vifaa maalum vitafungwa na itakuwa rahisi kujuwa ni wapi maji yanapotea na hivyo kuyadhibiti moja kwa moja.

Mradi huu unatekelezwa kwa gharama ya dola za kimarekani Milioni 32,927,222,45 kupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya India. 
Mh.waziri Lwenge akiwa katika zoezi la kukaguwa miradi ya maji ya Dawasa katika eneo la Kibamba jijini Dar es salaam.