WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa magari matatu yenye thamani ya Dola za Marekani 99,700 kutoka Kampuni ya Foton International Trade Co. Ltd ya nchini China.
Amepokea msaada huo leo (Jumatano, Agosti 9, 2017) jijini Dar es Salaam, ambapo amesema magari hayo yatatumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya jamii nchini. Magari hayo ni Sauvana SUV moja na Tunland Double cabin mbili.
“Nashukuru kwa msaada huu wa magari uliotolewa na Kampuni ya Foton kwa Serikali yetu. Magari haya yanaweza kutumika katika Hospitali za wilaya kwa ajili ya usambazaji wa dawa na vifaa tiba pamoja na kutolea elimu mbalimbali kwa umma.”
Pia, Waziri Mkuu ameikaribisha Kampuni hiyo kuja nchini kuwekeza katika ujenzi wa kiwanda cha kuunganisha magari. Amesema mbali na utulivu wa kisiasa uliopo Tanzania, pia kuna sera na mazingira mazuri ya uwekezaji.

Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Zhao Xiao amesema wametoa msaada huo wa magari kwa ajili ya kusaidia shughuli za maendeleo zinazofanywa na Serikali ya Tanzania hususan maeneo ya vijijini.
Bw. Xiao amesema Kampuni ya Foton inatengeneza magari 700,000 kwa mwaka, ambayo  yanauzwa katika nchi 125 duniani. Amesea ifikapo mwaka 2020 wanatarajia kuongeza uzalishaji na kufikia magari milioni 1.4 kwa mwaka.
Kuhusu suala la kuja kuwekeza kwenye ujenzi wa kiwanda cha kuunganisha magari nchini, Bw. Xiao amesema wanampango wa kuwekeza nchini kwa kuwa  kuna fursa nzuri za uwekezaji na uhakika wa masoko katika nchi zingine za Afrika Mashariki.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea Funguo za Magari matatu yenye thamani ya Dola za kimarekani 99,700 ambayo amekabidhiwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Foton International kutoka China Bwana Zhao Xiano Kwa ajili ya kusaidia shughuli za maendeleo nchini Tanzania, wanaoshuhudia kutoka kushoto  ni Meneja masoko wa kampuni ya Simba Motors Taanzania Bibi Ifigenia Salazar na kutoka kulia ni Afisa masoko wa Foton International, Bwana Fan Liang. Makabidhiano hayo yamefanyika leo ofisini kwa Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es salaam. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia moja ya magari aliyokabidhiwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Foton International kutoka China Bwana Zhao Xiano Kwa ajili ya kusaidia shughuli zamaendeleo nchini Tanzania Makabidhiano hayo yamefanyika leo ofisini kwa Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es salaam.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...