THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

WAZIRI MKUU AWAONYA WATU WANAOCHUKUA DAWA KATIKA HOSPITALI ZA SERIKALI NA KUZIPELEKA KATIKA MADUKA YAO.


Na Tiganya Vincent-RS-Tabora

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewaonya wamiliki wa maduka ya madawa ya binadamu na watumishi wa sekta ya afya wanaochukua dawa ambazo zinapaswa kupelekwa katika Hospitali za Serikali ili kuwahudumia wananchi na kuziweka katika maduka yao.

Mhe. Majaliwa alitoa kauli hiyo jana Wilayani Sikonge katika mkutano wa hadhara na wananchi katika Kiwanja cha TASAF.

Alisema kuwa vitendo hivyo ndivyo vimekuwa vikisababisha upungufu wa dawa katika Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali mbalimbali za Serikali na kufanya baadhi ya wananchi kuendelea kuteseka na maradhi kwa sababu ya kushindwa gharama za ununuzi wa dawa katika maduka ya watu binafsi.

Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa aliwaonya watumishi wa afya na wamiliki hao wenye tabia hizo kuacha mara moja endapo watabainika kuendesha vitendo hivyo watachukuliwa hatua kali.

Alisema kuwa Serikali inatumia fedha nyingi kwa ajili kununua dawa ili zinasaidia kutoa huduma ya matibabu kwa wananchi wake lakini kuna baadhi ya watumishi wa afya wasio waadirifu ambapo wamekuwa wakitorosha dawa na kuwauzia wamiliki wa maduka ya dawa na ksuababisha upungufu katika vituo vya Serikali.

Waziri Mkuu kuwa Serikali haiwezi kuwavilimia watumishi wa afya wasio waaminifu wanaochukua dawa na kuzipeleka katika maduka binafsi huku wakisababisha upungufu katika baadhi ya hospitali za umma.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Sikonge Mjini leo Agosti.10.2017 katika viwanja vya Tasaf Waziri Mkuu yupo Mkoani Tabora kwa ziara ya Kikazi .