THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

WAZIRI PROFESA MBARAWA AFANYA MAZUNGUMZO NA WADAU WA MAENDELEO NCHINI

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa tatu kulia), akizungumza na Rais wa Kampuni ya China Civil Engineering Construction Cooporation (CCECC) Bw. Zhao Dianlong kuhusu maendeleo ya ujenzi wa  barabara za maingiliano katika eneo la Ubungo (Ubungo interchange), leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa pili kulia), akizungumza na Makamu wa Rais wa kampuni ya China Harbour Engineering Company Ltd Bw. Liyi .. kuhusu upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Leo Jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa kampuni ya China Harbour Engineering Company Ltd Bw. Li-yi (Wa tatu kulia), akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Wa pili kushoto), kuhusu shughuli za Upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam, leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa pili kulia) akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzania  Bw. Song Geum-young (Kulia), kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na nchi yake hapa nchini.