Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amesema " Wote scheme ni Mkombozi kwa wananchi wengi walio katika Sekta isiyo rasmi na ameushahuri Mfuko wa Pensheni wa PPF kushirikiana na Maafisa Maendeleo ya Jamii kupitia Ofisi za Halmashauri ili kuweza kuwafikia kwa urahisi jamii ambayo haipo kwenye ajira rasmi na kuweza kunufaika na Mfumo huo.

Mfuko wa Pensheni wa PPF unashiriki  katika Maonesho ya Nane nane kitaifa Lindi kwa lengo la kuendelea kutoa elimu kwa wananchi  hasa  walio katika sekta isiyo rasmi kama vile wakulima, wafugaji, Wavuvi, wajasiriamali wakubwa na wadogo na wengine wote waliojiajiri wenyewe juu ya Mfumo wa " Wote scheme " ambao unawawezesha kujiwekea akiba wakati huo huo wakipata fursa za mafao ya Uzeeni, huduma za bima ya afya, mikopo ya maendeleo na mikopo ya kujiendeleza kielimu.

Vilevile kwa wale walioajiriwa wanaweza kumtumia Mfumo huu wa "Wote scheme"  kama mfumo  wa hiari wa kujiwekea akiba Zaida Mahava, Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya kusini amesema kwa kutambua kundi kubwa la jamii ambalo halipo kwenye ajira rasmi wameona ipo haja ya kutoa elimu juu Mfumo wa Wote scheme ili waweze kunufaika na huduma zinazotolewa na PPF kupitia Mfumo wa Wote scheme.
 Naibu Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Angelina Mabula (Mb) akiongea jambo na Meneja wa PPF Kanda ya Kusini Bi Zaida Mahava (kushoto) pamoja na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF baada ya kupewa maelezo ya namna ya Mfumo wa WOTE SCHEME unavyofanya kazi na faida zake kwa sekta isiyo rasmi wakati alipotembelea Banda la PPF lililopo chini ya banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Kilimo Nane Nane 2017 yanayofanyika Kitaifa Lindi katika Viwanja vya Ngongo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
 Meneja wa PPF Kanda ya Kusini Bi Zaida Mahava akimuelekeza Mwananchi jinsi ya kujaza fomu ya kujiunga na mfumo wa hiari wa Wote scheme baada ya kupewa elimu alipofika katika Banda la PPF lililopo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika Kitaifa Lindi katika Viwanja vya Ngongo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.
 Naibu Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Angelina Mabula (Mb) alipotembelea banda la PPF lililopo chini ya banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Kilimo Nane Nane 2017 yanayofanyika Kitaifa Lindi katika Viwanja vya Ngongo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
Naibu Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Angelina Mabula (Mb) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la PPF lililopo chini ya banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Kilimo Nane Nane 2017 yanayofanyika Kitaifa Lindi katika Viwanja vya Ngongo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...