Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii
CHUO Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi Muhimbili kupitia Shule ya Famasi kwa kushirikiana kwa Kituo cha cha Mafunzo ya Kutathimini Dawa cha Afrika Mashariki wameendesha mafunzo ya kutathimini kwa ulinganifu ufanisi , Ubora na usalama wa dawa katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Shirika la Afya Duniani (WHO) na Sekeretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wameshiriki katika uratibu wa mafunzo hayo na kutoa misaada ya hali na mal.i
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto , Dk. Ulisubisya Mpoki amesema mfumo kutathimini dawa za Afrika Mashariki ni muhimu katika kuhakikisha kuwa wananchi wa ukanda huo wanapata dawa bora, salama na zenye ufanisi mkubwa.
Dk. Mpoki amesema mafunzo hayo ya nadharia na vitendo kwa wataalam wa dawa wa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki yanalenga kuhakikisha kuwa dawa zote zilizokidhi vigezo zinasajiliwa kwa mfumo wa ulinganifu unaotumika baada wataalam hao kujiridhisha kisayansi.
Nae Mkuruenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Bw. Hiiti Sillo amesema kuwa kumekuwa na ushirikiano wa karibu na wananchi katika utoaji wa taarifa pale wanapoona kuna dawa zenye mashaka ziko mtaani, hivyo kusaidia katika dhima ya kulinda afya ya jamii.
Amesema kuwa kuanzishwa kituo cha kutathimini Dawa cha Afrika Mashariki kitakuwa ni msaada mkubwa katika kuhakikisha kuwa kila dawa zilizo katika nchi za Afrika Mashariki ni zilizosajiliwa na usajili kwa matumizi ya wananchi wote wa ukanda husika.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki akizungumza katika
ufunguzi wa mafunzo ya kutathimini kwa ulinganifu ufanisi , Ubora na
usalama wa dawa katika ukanda wa Afrika
Mashariki yalifanyika leo jijini Dar es Salaam,
Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TFDA , Hiiti Sillo , Kulia ni Mkurugenzi wa
Shahada za awali wa MUHAS, Profesa
Mainen Moshi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Chakula na Dawa (TFDA), Hiiti Sillo akizungumza na waandishi wa habari juu ya mafunzo ya
kutathimini kwa ulinganifu ufanisi , Ubora na usalama wa dawa katika ukanda wa Afrika Mashariki leo jijini Dar es Salaam
Mratibu wa Mafunzo wa MUHAS –TFDA , Profesa Eliangiriya Kaale akitoa neno la shukrani baada ufunguzi
wa mafunzo
ya kutathimini kwa ulinganifu ufanisi , Ubora na usalama wa dawa katika ukanda wa Afrika Mashariki leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki akiwa katika
pamoja na Maprofesa wa Chuo cha Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi pamoja na Watalaam
leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...