Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza katika Kituo cha Forodha Bandarini, kilichoko katika Bandari ya Dar es Salaam na kuiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, kufanya mabadiliko makubwa ya watumishi walioko katika idara ya upimaji na ukaguzi wa mizigo baada ya kubainika kuwa baadhi yao wanajihusisha kwa namna moja au nyingine na upotevu wa mapato ya Serikali.

Dokta Mpango ametoa muda wa siku saba kwa TRA kumpa taarifa kamili ya utekelezaji wa maagizo hayo, ikiwemo kuwahamisha watumishi wote waliokaa muda mrefu kwenye eneo hilo la upimaji na ukaguzi wa mizigo ili kuongeza ufanisi wa ukusanyaji mapato ya Serikali katika Bandari hiyo.

Ameshangazwa na kitendo cha Mapato katika Bandari ya Dar es Salaam kutoongezeka licha ya juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano, kuboresha Bandari hiyo kutokana na baadhi ya watumishi wasio waaminifu kushirikiana na wafanyabiashara wasio waaminifu kukwepa kodi ya serikali.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia) akiwa katika kikao na Maafisa Waandamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) alipofanya ziara ya kukagua utendaji ambapo aliwataka kuchukua hatua dhidi ya watumishi wasiowaaminifu wanaolikosesha Taifa mapato stahiki.
Meneja wa Idara ya Forodha, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bandari ya dar es Salaam, Bw. John Micah (kulia) na Meneja anaye husika na suala la Mafuta Bw. Stephen Malekano (kushoto) wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (hayupo pichani) alipofanya ziara Idara ya Forodha, Bandarini, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa Maafisa waandamizi wa Mamlaka ya mapato Tanzania-TRA, alipofanya ziara ya kushitukiza bandari ya Dar es Salaam na kuagiza kitengo cha ukaguzi na upimaji wa mizigo bandarini kifumuliwe baada ya watumishi wake kutofanyakazi ya kukusanya mapato ya Serikali ipasavyo
Afisa Kitengo cha Bandari Majahazi, Bw. Mahmood Makame, akifafanua jambo mbele ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) kuhusu changamoto ya elimu kuhusu masuala ya kodi kwa wateja wanaotumia Bandari ya Dar es Salaam, alipofanya ziara ya kushitukiza katika ofisi hiyo.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...