THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

DOKTA MPANGO AIHIMIZA UINGEREZA KUKUZA ZAIDI BIASHARA NA UWEKEZAJI NCHINI

Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam.

Tanzania imetoa rai kwa Serikali ya Uingereza kubadili mfumo wa uhusiano wake kwa kujikita zaidi katika masuala ya biashara na uwekezaji badala ya kutoa misaada ya kawaida ili nchi iweze kukuza uchumi wake kwa haraka zaidi.

Wito huo umetolewa Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango, alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa wabunge kutoka mabunge ya uingereza (Baraza la Mamwinyi na Bunge la Wawakilishi).

Dokta Mpango amesema kuwa kiwango cha mtaji ambacho Serikali ya Uingereza imewekeza nchini hadi sasa ni Paundi bilioni 2.5 lakini kwa upande wa biashara kati ya nchi hizo mbili, hali si nzuri.

"Mwaka 2015 Tanzania iliuza nje bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 22.5 na kununua bidhaa kutoka Uingereza zenye thamani ya Dola milioni 150, kiwango ambacho ni kidogo sana na tunahitaji kufanya biashara zaidi" Alisisitiza Dkt. Mpango.

Alielezea hatua mbalimbali ambazo Serikali inazichukua kuimarisha uchumi wa viwanda na kuelezea changamoto kubwa ikiwa na namna ya kuendeleza kilimo kwa ajili ya kupata malighafi za viwanda na kuwainua wananchi kiuchumi kwa kuwa kilimo ndicho kinaajiri idadi kubwa ya Watanzania.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa tatu kushoto), akiongoza majadiliano na Ujumbe wa Wabunge watano pamoja na maafisa kadhaa kutoka nchini Uingereza, walipomtembela na kufanya naye mazungumzo Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wabunge wa mabunge ya Uingereza wakiwa katika kikao na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt, Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), akisisitiza jambo alipokutana na kufanya mazungungumzo na wabunge kutoka nchini Uingereza waliomtembelea Jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Kaimu Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Mamelta Mutagwaba.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akizungumza na Wabunge kutoka Nchini Uingereza waliomtembelea katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na kuipongeza nchi hiyo kwa kuisadia Tanzania katika masuala mbalimbali, amesisitiza ushirikiano wa nchi hizo mbili ujikite zaidi katika masuala ya biashara na uwekezaji.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kushoto) na Kiongozi wa Ujumbe wa Wabunge kutoka Uingereza, Mhe. David Linden (katikati) na Wabunge wengine kutoka Uingereza, Maafisa Waandamizi kutoka Tanzania, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa Mkutano katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA