Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka wadau wa sekta ya ujenzi kuanza kuweka twakwimu takwimu zinazohusu masuala ya ujenzi hapa nchini.

Akifungua warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Prof. Mbarawa, amesisitiza umuhimu wa sekta hiyo kuimarisha taarifa za aina, vifaa, viwango vinavyohitajika kimataifa na gharama katika shughuli za ujenzi wa barabara, viwanja vya ndege, nyumba na miundombinu mingine.

“Sekta ya Ujenzi ina mchango mkubwa katika ujenzi wa miundombinu ya kiuchumi na kijamii hivyo uwepo wa taarifa mbalimbali unahitajika ili kurahisisha uelewa wa wananchi wa kawaida katika masuala ya ujenzi na gharama zake”, amesema Prof. Mbarawa.

Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amewahakikishia wadau wa sekta ya ujenzi kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili kuhakikisha sekta hiyo inakidhi matarajio ya watanzania wengi kwa lengo la kuwajengea miundombinu iliyo bora na imara.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akihutubia wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini Dar es Salaam.
Wadau wa sekta ya ujenzi wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani), katika warsha ya sekta hiyo kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga (kulia), katika warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...