Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack amezindua kampeni ya upandaji miti katika wilaya ya Shinyanga yenye kauli mbiu ya ‘Shinyanga Mpya,Mti Kwanza’ ili kuboresha mazingira Shinyanga na kupambana na mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha jangwa. 

Kampeni hiyo inayoratibiwa na ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, imezinduliwa leo Jumamosi Septemba 23,2017 katika manispaa ya Shinyanga ,kwa lengo la kuboresha mazingira ya mji wa Shinyanga,maeneo ya taasisi,maeneo ya wazi,maeneo yanayozunguka kaya,kandokando ya barabara na sehemu zingine ambazo hazina miti. 

Akizungumza wakati wa kuzindua kampeni hiyo,Telack alisema kutokana na mvua haba katika mkoa wa Shinyanga, kumekuwepo na mabadiliko ya tabia nchi hali inayosababisha kuwepo na hali ya jangwa. Telack aliwataka wananchi na wadau wote kuhakikisha wanatunza miti hiyo na kuzuia mifugo kuzurura ovyo mitaani. 

“Tutakuwa wakali,kuanzia sasa ni marufuku kwa mifugo kuzurura mitaani,ikikamatwa kwa kila mfugo faini ni kati ya shilingi 50,000/= na 100,000/=,iwe ng’ombe,mbuzi,kondoo au punda, tukikuta mti umekauka faini ni shilingi 50,000/=”,alieleza mkuu huyo wa mkoa. 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akizungumza wakati wa kuzindua kampeni ya upandaji miti ‘Shinyanga Mpya,Mti Kwanza’ leo katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga.Kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga,Geofrey Mwangulumbi.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro wakati wa uzinduzi huo. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ya upandaji miti ambapo alisema miongoni mwa malengo yake ni kuhifadhi ardhi na kuiongezea thamani,kuzuia mmomonyoko wa adhi na kuboresha mazingira
Wananchi wakiwa wameshikilia vijiti vinavyotumika katika zoezi la upandaji miti.
Uzinduzi unaendelea
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akichomeka vijiti kwenye mti aliopanda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...