Na Muhidin Amri, Songea.
MFUKO wa taifa wa Bima ya Afya(NHIF) umewahimiza wana michezo nchini kuchangamkia fursa ya kujiunga na mpango wa matibabu kupitia mfuko wa afya ya jamii(CHF) na mfuko wa taifa wa Bima ya Afya(NHIF) kwa ajili ya kupata huduma bora za matibabu pindi wanapoumia wakiwa michezoni.

Rai hiyo imetolewa  mwishoni mwa wiki na meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF)mkoani Ruvuma Abdiel Mkaro wakati wa Bonanza maalum la kuhamasisha jamii hususana wana michezo kujiunga na mfuko huo na kushiriki mazoea mara kwa mara ili kuepuka uwezekano wa kupata magonjwa yasiokuwa ya lazima.

Aliwataka wana michezo na jamii ya watanzania wakiwemo waandishi wa habari,kuona umuhimu wa kijunga na mpango huo  kwa lengo la kuwa na uhakika wa matibabu  pale  inapotokea kupata ajali na magonjwa ya kawaida.

Bonanza hilo liliandaliwa na NHIF lilishirikisha michezo mbalimbali kama vile kukimbia,mazoezi ya viungo,kukimbiza kuku pamoja na mpira wa miguu ambap timu ya soka ya Mkambi FC ilifanikiwa kuibuka mshindi baada ya kuifunga timu ya NHIF 4-2 kwa njia ya Penalti kufuatia matokeo ya kufungana 1-1 ndani ya Dkt 90 za mchezo huo.

Hata hivyo Bonanza hilo lililoonekana kuvutia watu wengi kutoka maeneo mbalimbali ya manispaa ya Songea, baadhi ya washiriki  wameiomba Nhif kuendelea kuandaa bonanza kama hilo kila mwiso wa mwezi ili kutoa fursa kwa wananchi kushiriki na kufanya mazoezi ili kuepusha uwezekano wa kupata magonjwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...