Mwanamuziki nguli wa miondoko ya Bongo Fleva nchini Ali Kiba amesema moja ya mafanikio anayojivunia nayo katika kazi ya muziki kwa mwaka huu ni ushiriki wake tena katika onyesho la Coke Studio msimu wa mwaka huu. Ali Kiba ambaye amefanya kolabo kwa kushirikiana na mwanamuziki nguli kutoka Nigeria, Patoranking, amesema katika mahojiano hivi karibuni kuwa anajivunia kuwa miongoni mwa wanamuziki wanaoshiriki kwenye msimu wa tano wa Coke Studio unaoendela ambapo kwa hapa nchini onyesho lake linarushwa na luninga ya Clouds kila Jumamosi saa 12 jioni. 

 Anasema ushiriki wake kwa mara ya moja ya kwenye mafanikio kwani rekodi yake imezidi kuongezeka katika anga la kimataifa na ameweza kujiongezea washabiki ambao wanafuatilia shindano hili kupitia luninga,vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Mbali na kuongelea mafanikio ya kupata washabiki amesema kuwa amefurahi kufanya kolabo na msanii wa nje ya nchi kwa kuwa ameweza kujifunza mengi kupitia ushiriki wake kwenye Coke Studio.
“Jambo lingine ambalo naliona ni kubwa kama msanii ni kukubalika kufanya kazi na kampuni kubwa kama Coca Cola kazi hii imenifanya nizidi kujiongezea mashabiki na umaarufu wangu kuongezeka”Alisema. Alisema onyesho la Coke Studio linadhihirisha kuwa muziki wa Bongo Fleva unazidi kukua na kuwa maarufu sehemu mbalimbali barani Afrika kutokana na jinsi linavyofuatiliwa na idadi kubwa ya watu hususani vijana. 

 Aliwataka wanamuziki wachanga wanaochipukia kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha wanapata mafanikio na kuongeza kuwa mafanikio yanapatikana kwa kufanya kazi na makampuni makubwa ya biashara mojawapo ikiwa ni kushiriki kwenye maonyesho makubwa kama haya. “Fani ya muziki inazidi kukua kiasi kwamba wakati wa kufanya muziki wa ndani tu imekwisha na inabidi kuvuka mipaka na kolabo kama hizi za Coke Studio zinasaidia kupata uzoefu na kufungua milango ya mafanikio”.Alisema. Alimalizia kwa kuwapongeza wanamuziki wenzake kutoka Tanzania ambao yuko nao katika msimu wa Coke Studio mwaka huu.Wanamuziki hao ni , Rayvanny, Izzo Bizness, na Nandy.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...