Na. Paschal Dotto- MAELEZO.

Serikali ya Awamu ya Tano chini ya  uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza vitendo vya rushwa katika ofisi za Serikali, taasisi na mashirika ya umma na kuweka usawa katika  upatikanaji wa huduma kwa jamii.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam  na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John  Mbungo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kuhusu rushwa katika taasisi na mashirika ya umma kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.

 Brigedia Jenerali Mbungo alisema kuwa lazima watumishi wajifunze kuwa waadilifu, kwa hiyo kile watakachokipata kutoka katika mkutano huo kikafanye kazi kuleta haki kwa wananchi wakati wa kupata huduma katika ofisi zao ili kuendana na sera ya Awamu ya Tano ya kutokuvumilia vitendo vya rushwa nchini.

“Tumieni fursa katika kikao hiki ili kuweza kupata elimu itakayosaidia wananchi kuelimika juu ya vitendo vya rushwa na kupata haki zao za msingi wanapopata huduma katika ofisi zenu”,alisema Brigedia Jenerali Mbungo.
Kikao kazi hiki ni cha kwanza ambacho kinafuatia mkakati wa awamu wa tatu  utakaokuwa wa miaka mitano kuanzia  Julai, 2017 unaolenga kuanzia ngazi za vijiji, wilaya, mkoa, mpaka taifa ili kudhibiti uadilifu, nidhamu na utendaji kazi wenye kuzingatia haki katika ofisi mbalimbali nchini.

Aidha Brigedia Mbungo alisema kuwa kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na serikali, hali ya rushwa nchini imepungua kwa kiasi kikubwa kwani malalamiko yamepungua katika ofisi, taasisi na mashirika ya umma.

“Hali ya rushwa sasa hivi imepungua kwa sababu Serikali kwa kutumia juhudi  mbalimbali imedhibiti hali hii, Tanzania ina viwango vya chini sana vya rushwa ikilinganishwa na nchi nyingine za maziwa makuu kwa hiyo naweza kusema kiwango kimepungua sana hususani kwa Jiji la Dar es Salaam ambapo vitendo hivi vilishamiri sana, hivyo katika awamu hii ya tatu ya mkakati huu tunatarajia viwango vitashuka zaidi”, alisisitiza Brigedia Jenerali Mbungo.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbungo akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wajumbe wa Kamati za kudhibiti uadilifu kuhusu utekekelezaji wa mkakati wa taifa dhidi ya rushwa, awamu ya tatu (2017-20120) leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bibi. Theresia Mmbando na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Bw. Edward Mpogolo.
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bibi. Theresia Mmbando akielezea jambo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wajumbe wa Kamati za kudhibiti uadilifu kuhusu utekekelezaji wa mkakati wa taifa dhidi ya rushwa, awamu ya tatu (2017-20120) leo jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Kitengo cha Utawala Bora kutoka Ofisi ya Rais Bi. Christina Maganga akitoa neno la utangulizi kuhusu mkakati wa taifa dhidi ya rushwa awamu ya tatu wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wajumbe wa kamati za kudhibiti uadilifu kuhusu utekekelezaji wa mkakati huo leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kudhibiti uadilifu kutoka mkoa wa Dar es Salaam wakifuatilia wakifuatila mada wakati wa kikao kazi cha wajumbe wa kamati hizo kuhusu utekekelezaji wa mkakati wa taifa dhidi ya rushwa, awamu ya tatu (2017-20120) leo jijini Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...