Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Mkame Mbarawa ameitaka Bodi Mpya ya Wakurugenzi ya kampuni ya mawasiliano nchini (TTCL) kuhakikisha kuwa inasimamia vyema kazi na majukumu yake ili kuiwezesha kampuni hiyo kujiendesha kibiashara na kuimarisha huduma za mawasiliano hapa nchini.

Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo ambapo aliwasisistiza kuwa wachape kazi ili kurahisisha huduma mbalimbali za kimawasiliano hapa nchini na kuhakikisha kuwa wanaendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano yenye sera ya hapa kazi tu.

“Nataka bodi mjue tunakwenda wapi katika kampuni hii lakini pia tunahitaji kufanya kazi kwa juhudi, kushindana na makampuni mengine ya simu, mhakikishe mapato makubwa yanatoka kwenye data halikadhalika tujue mnapaswa mjue strenght (nguvu) yenu iko wapi maana tusipojibu maswali haya hatuwezi kufanya ushindani na makampuni mengine,” alifafanua Prof. Mbarawa.

Aidha Prof. Mbarawa alisema kuwa, Serikali imeweka sera nzuri za uwekezaji katika sekta ya mawasiliano kiasi ambacho kimeongeza mapato pamoja na ushindani wa huduma ya mawasiliano na kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi na maendeleo hapa nchini.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo mbele ya wajumbe wa Bodi ya Kampuni ya Simu ya TTCL katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) Dkt. Maria Sasabo na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhandisi Omary Nundu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Simu za Mkononi ya TTCL Mhandisi, Omary Nundu akielezea jambo wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Mawasiliano) Dkt. Maria Sasabo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya mawasiliano) Dkt. Maria Sasabo akizungumza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Bodi ya Kampuni ya Simu ya Mkononi ya TTCL leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TTCL, Bw. Waziri Kindamba, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Mhandisi Omary Nundu na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya TTCL wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.Picha na Frank Shija – MAELEZO



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...