MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amezindua
rasmi wa Ufyatuaji wa Matofali kwaajili ya ujenzi wa ofisi za kisasa 402 za
Walimu ambapo amewasihi Wadau na Wananchi kuunga Mkono jitiada hizo.
Katika uzinduzi huo
RC Makonda ameshiriki zoezi la Ufyatuaji wa Matofali kwaajili ya Ujenzi
huo.
Makonda amesema lengo la Ujenzi wa Ofisi hizo ni
kuboresha Mazingira ya kufanya kazi kwa walimu ili waweze kutoa Elimu bora kwa
Wanafunzi na kuongeza ufaulu.
Amesema wapo wengi waliopanga kufanya ujenzi wa Ofisi za
Walimu lakini mipango hiyo iliishia kubaki kwenye makarabrasha maofisini lakini
kupitia juhudi zake na Kamati aliyoiunda wameweza kuleta matokeo chanya.
RC Makonda ametoa wito kwa Wananchi na Wadau kuchangia
Mabati, Saruji, Kokoto,Mchanga, Nondo au Nguvu kazi ilikuwawezesha walimu
kufanyakazi katika mazingira bora.
Amesema ataki kuona kwenye Mkoa wake Walimu wanadhalilika kwa kukosa Ofisi na Vyoo hali
inayopelekea kujisaidia kwa Majirani,Bar au Vichakani.
Aidha amesema hadi sasa amefanikiwa kupata mifuko zaidi
ya 10,000 ya Saruji Mashine za kufyatulia Matofali,Gurdoza na vifaa vingine
ambapo ataendelea kugonga hodi kwa Wadau ili waweze kuchangia ujenzi huo.
Amewaomba Wananchi kuwa na uzalendo kwa kujitoa katika
ujenzi huo iwe kwa mtu binafsi au Vikundi vya Joaging,Timu za Mpira na vikundi
vya maendeleo.
Ameipongeza Kamati ya ujenzi wa Ofisi za walimu,JKT,Jeshi
la Magereza, Jeshi la Polisi,NHC, TBA,Channel Ten na Umoja wa Wamiliki wa
Malori na wengine kwa namna wanavyojitoa kusaidia katika zoezi hilo.
Katika hatua nyingine RC Makonda amesema atatoa TV 30 kwa
Magereza ya Ukonga, Segerea na Keko ili wafungwa wapate fursa za kutazama
hotuba za Rais Dk. John Pombe Magufuli ili wajue maendeleo yanayofanyika
uraiani.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Ofisi
za Walimu Canal Charles Mbuge amesema hadi sasa kiasi cha fedha kilichotumika
ni zaidi ya Million 200 ambapo watahakikisha ujenzi huo unakamilika.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizugumza leo katika uzinduzi wa Ufyatuaji wa Matofali kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za kisasa 402 za Shule katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu Kanali Charles Mbuge akizungumza katika uzinduzi wa ufyatuaji tofali za ujenzi wa ofisi za shule katika mkoa wa Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akishiriki wa Ufyatuaji wa Matofali kwaajili ya ujenzi wa ofisi za kisasa 402 leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanel Massaka,Globu ya Jamii).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...