Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amewataka Watanzania kuenzi na kuimarisha utamaduni wao ili kuepukana na chamgamoto ya utamaduni kutoka nchi za magharibi unaoletwa ukuaji wa sayansi na teknolojia.

Prof. Elisante ametoa kauli hiyo leo Tukuyu wakati wa ufunguzi wa tamasha la Ngoma za jadi linaloratibiwa na Taasisi ya Tulia Trust inayoongozwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson inayojishughulisha na masuala ya kukuza na kuendeleza utamaduni nchini.

Prof. Elisante amewahakikishia vijana kuwa kuwekeza mahali salama, hivyo waendelee kukuza sanaa yao iweze kujijengea jina na kutambulika ndani na nje ya nchi.“Vijana muendelee kuthamini utamaduni wetu, tusiposimamia, kuwekeza na kuthamini utamaduni wetu, utamaduni wan chi za magharibi utawachukua vijana wetu na kuacha tunu yetu ya asili tangu enzi za babu zetu” alisema Prof. Elisante

Prof. Elisante amewahakikishia waandaaji wa tamasha hilo kuwa Serikali ipo sambamba nao na kuwataka wapanue wigo wa tamasha hilo ili liweze kuwa na matawi na kuwafikia watu wengi zaidi nchi nzima.Akifungua tamasha hilo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala amesema limekuwa kichocheo cha kukuza na kuendeleza utamaduni wa Mtanzania hatua inayoongeza fursa ya ajira kwa vijana mkoani Mbeya. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyevaa mashuka ya Kimasai) akiongea na washiriki wa tamasha la Ngoma za jadi linaloratibiwa na Taasisi ya Tulia Trust leo wilayani Tukuyu mkoani Mbeya. Wa kwanza kushoto ni Mwasisi wa taasisi hiyo ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala akifungua tamasha la ngoma za jadi leo wilayani Tukuyu mkoani humo ambapo amesisitiza Watanzania kukuza na kuendeleza utamaduni wa Mtanzania hatua inayoongeza fursa ya ajira kwa vijana mkoani humo.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akipokea zawadi ya CD kutoka kwa Mchungaji Damian Matipa wa Kanisa la Uponyaji Mbeya Mjini yenye nyimbo za kumpongeza Naibu Spika kwa kazi anazofanya.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel mara baada ya kuwasili Tukuyu mkoani Mbeya.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiteta jambo na Mkuu wa Majeshi Mtaafu Jenerali Davis Mwamunyange wakati wa tamasha la Ngoma za jadi linaloratibiwa na Taasisi ya Tulia Trust leo wilayani Tukuyu mkoani Mbeya.
Ngoma ya Bugobo gobo kutoka Bujara mkoani Mwanza
Baadhi ya viongozi wakiwa wamebeba moja ya vifaa Bugoyangi (nyoka) vinavyotumiwa na kikundi cha kucheza ngoma cha Bujora mkoani Mwanza.
Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Tukuyu, Mbeya.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...