Na. Neema Mathias- MAELEZO

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imeandaa tamasha la 36 la Kimataifa kuanzia tarehe, 23 hadi 30, Septemba litakalofanyika katika viwanja vya taasisi hiyo mjini Bagamoyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo Dkt.Hebert Makoye alisema kuwa tamasha hiyo litakuwa na kauli mbiu isemayo ‘sanaa na utamaduni katika kupiga vita madawa ya kulevya’.

“Kauli mbiu hii ni mahsusi katika kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli za kupiga vita matumizi na usambazaji wa dawa za kulevya nchini” alisema Dkt. Makoye.

Aliongeza kuwa wakati wa tamasha elimu ya kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya itatolewa ikiwalenga hasa vijana ambao ndio waathirika wakuu wa dawa hizo ambapo kutakuwa na midahalo na makongamano kuhusu athari za matumizi ya dawa hizo.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) (wa pili kushoto) akiongea na Waandishi wa habari kuhusu kufanyika kwa Tamasha la Kimataifa la 36 linalohusu Sanaa na Utamaduni Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) 21 Septemba, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tamasha la Sanaa na Utamaduni toka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) (kushoto) akitolea ufafanuzi kwa Waandishi wa habari kuhusu kufanyika kwa Tamasha la Kimataifa la 36 linalohusu Sanaa na Utamaduni Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) 21 Septemba, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakichukua taarifa wakati wa Mkutano wa Waandishi wa habari uliohusu kufanyika kwa Tamasha la Kimataifa la 36 linalohusu Sanaa na Utamaduni Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) 21 Septemba, 2017 Jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM


………………………………..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...