Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi (aliyesimama) akizungumza na wadau kutoka Asasi mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya vijana alipokua akifungua kikao cha kupitia mwongozo wa Stadi za Maisha wa mwaka 2009 kwa vijana walio nje ya shule leo Jijini Dar es Salaam.

Na Genofeva Matemu - Maelezo 

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu imewakutanisha wadau mbalimbali kutoka Asasi zinazojishughulisha na masuala ya vijana ili ziweze kushirikiana na serikali kupitia na kuboresha Mwongozo Sanifu wa Stadi za Maisha kwa Vijana kwa kubadilishana uzoefu walionao na kuuwezesha mwongozo huo kumsaidia kijana katika mazingira ya sasa.

Akifungua kikao cha wadau hao Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi amesema kuwa msingi mkubwa wa kuboresha mwongozi sanifu wa stadi za maisha kwa vijana ni pamoja na kuangalia namna gani serikali inaweza kuwasaidia vijana kwa kuwawezesha kujitambua, kujiendeleza wenyewe na kukuza uchumi wa nchi yetu.

"Mwongozo wa stadi za maisha umekua ukiwajenga vijana kwa kuwaandaa kujitambua ili waweze kuhimili changamoto mbalimbali zilizopo kama vile vishawishi mbalimbali vinavyowakabili, magonjwa, matumizi ya madawa ya kulevya, mimba za utotoni pamoja na ukosefu wa ajira" amesema Bw. Shitindi kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi amesema kuwa kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia, kiuchumi, kisayansi na kijamii serikali imeona ni vyema kukaa pamoja na wadau hao kuangalia yale yaliyomo kwenye Mwongozo wa mwaka 2009 na kufanya uchambuzi yakinifu kwa kila eneo ndani ya mwongozo huo.

aidha Bw. Kajugusi amewashukuru wadau kutoka Asasi mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya vijana kwa kuisaidia serikali kufikisha elimu ya stadi za maisha kwa vijana kulingana na mipango na programu zao na kuwahaidi kuendelea kufanya nao kazi katika kujenga taifa lenye vijana wanaojitambua.

Naye Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Shirika la Kimataifa la Idadi ya watu Bibi. Tausi Hassan ameishukuru serikali kuwakutanisha wadau wanaofanya kazi na vijana moja kwa moja kushirikiana katika kuboresha Mwongozo wa Stadi za Maisha kwa vijana kwani ushirikiano huo utalenga nyanja zote hivyo kupata mwongozo unaokidhi matakwa ya vijana kitaifa.
Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi (katikati) akifafanua jambo wakati wa kikao na wadau kutoka Asasi mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya vijana kupitia mwongozo wa Stadi za Maisha wa mwaka 2009 kwa vijana walio nje ya shule leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi Ushauri Nasaha Bw. Juma Mswadiku (kushoto) akitoa hoja wakati wa kikao na wadau kutoka Asasi mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya vijana kupitia mwongozo wa Stadi za Maisha wa mwaka 2009 kwa vijana walio nje ya shule leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha kupitia mwongozo wa Stadi za Maisha wa mwaka 2009 kwa vijana walio nje ya shule wakifuatilia mada zilizokua zikiendela leo wakati wa kikao na wadau kutoka Asasi mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya vijana.
Mwezeshaji kutoka Chama cha Stadi za Maisha (LISA) Bw. Elemeth Oloo akitoa mada kwa wadau kutoka Asasi mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya vijana wakati wa kikao cha kupitia mwongozo wa Stadi za Maisha wa mwaka 2009 kwa vijana walio nje ya shule leo Jijini Dar es Salaam. Picha na: Genofeva Matemu - Maelezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...