Na: Lilian Lundo – MAELEZO Dodoma.

Wafanyakazi nchini wameshauriwa kupima afya zao mara tu wanapostaafu ili kujihakikishia ikiwa hawajaathirika na kazi ambazo wamekuwa wakizifanya.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Eric Shitindi alipokuwa akifungua semina ya viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) na viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi juu ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi, leo Mjini Dodoma.

“Kumekuwa na mazoea kwa wafanyakazi kupima Afya pale tu wanapoajiriwa na kutotilia maanani upimaji afya zao mara wanapostaafu ili kujua ikiwa kazi wanazozifanya zimewaathiri kwa kiasi gani,” amesema Shitindi.

Ameendelea kwa kusema kuwa, upimaji wa afya mara baada ya kustaafu utasaidia watumishi kujua afya zao na ikiwa watakuwa wameathirika upitia kazi walizokuwa wakizifanya basi mwajiri atawajibika mkulipa fidia mtumishi huyo.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) Bi. Khadija Mwenda akiongea na Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(TUCTA) na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wakati wa Ufunguzi wa Semina kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi Leo Mjini Dodoma.Kulia ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw.Qambos Sule
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi akiongea na Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(TUCTA) na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wakati wa Ufunguzi wa Semina kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi ambapo aliwashauri wafanyakazi nchini kupima afya mara wanapostaafu ili kujihakikishia kama hawajaathirika na kazi walizokuwa wanafanya.Katikati ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw.Qambos Sule na Kushoto ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) Bi. Khadija Mwenda 
 Makamu wa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw.Qambos Sule akiongea naViongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(TUCTA) na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wakati wa Ufunguzi wa Semina kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi, kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi na kushoto ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) Bi. Khadija Mwenda.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...