Wananchi wa Wilaya ya Kilolo wameendelea kujitokeza kwa wingi kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa baada ya kukamilisha awamu ya kwanza ya usajili ambayo ni kujaza fomu za maombi ya Usajili na fomu zao kupitishwa na Serikali za Vijiji wanakoishi.

Zoezi linaenda sambamba na uhakiki wa taarifa za wananchi wanaoomba kupewa vitambulisho vya Taifa chini ya Kamati za Ulinzi na Usalama ngazi ya Mitaa na Vijiji kabla ya kutoa nafasi kwa wananchi kuweka Mapingamizi ya wazi kwa wale waombaji wanaotiliwa shaka uraia wao kabla ya kuendelea na mchakato wa Uzalishaji.

Wilaya ya Kilolo ni Wilaya ya mwisho kukamilisha zoezi hili kwa mkoa wa Iringa na hivyo kutoa fursa ya kuanza kwa matumizi ya Vitambulisho vya Taifa kielektroniki.

Mbali na Iringa mikoa mingine inayoendelea na zoezi hilo ni ya Kanda ya Ziwa ikiwemo; Geita, Shinyanga, Mwanza, Manyara na Singida.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika chumba cha usajili tayari kusajiliwa.


Hawa ni baadhi tu ya wananchi waliojitokeza katika zoezi la Usajil Vitambulisho vya Taifa Wilaya ya Kilolo mkoa wa Iringa. Kwa sasa zoezi hili linafanyika kwa awamu ngazi ya Kata ili kutoa fursa kwa wananchi wote wenye sifa kusajiliwa.
Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa akiingiza taarifa za wananchi kwenye mfumo kabla ya kuchukua taarifa za kibaiolojia za wananchi wa Kilolo ambako zoezi kwa sasa linaendelea.
Mmoja wa wananchi akichukuliwa alama za vidole na saini ya kielektroniki ikiwa ni hatua muhimu kabla ya kukamilisha hatua za Usajili Vitambumnbulisho vya Taifa. Mkoa wa Iringa ni moja ya Wilaya zinazo endelea na Usajili kwa sasa kati ya mikoa 11 ya Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...