THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Wataoanza kampeni mapema katika uchaguzi wa Jumuiya wazazi wajiandae kukatwa majina- Bulembo.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
JUMUIYA ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema wagombea ambao wataanza kampeni kabla ya muda wajiandae kukatwa majina yao.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Abdallah Bulembo amesma kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kinaendeshwa na kanuni hivyo waombea wasipofuata kanunni hizo lazima wawe na roho ngumu pindi wanapokatwa majina yao.

Amesema makatibu wa Wilaya na Mikoa katika maeneo yao ikibainika kuwepo kwa rushwa katika uchaguzi wa jumuiya hizo ajira zao ziko mashakani kuweza kuondolewa katika nafasi na kuwapa watu wenye weledi.
Bulembo amesema katika uchaguzi huo kwa ngazi ya taifa hagombei na kazi yake itakuwa kuwachuja wagombea 49 waliogombea nafasi ya wenyekiti taifa.

Amesema katika uongozi wake aliikuta akaunti ya jumuiya hiyo ikiwa na sifuri lakini sasa akaunti hiyo ina fedha  ambayo ataikabidhi baada ya uchaguzi huo kufanyika.

Mwenyekiti huyo amesema katika uongozi wake amepima viwanja 56000 vya jumuiya ya wazazi , uimarishaji wa shule ambazo zilikuwa zinaendeeshwa kama mali binafsi.

Bulembo amesema kuwa katika mazoea ya uongzozi wake ni kutumikia kipindi kimoja ili aweze kukumbukwa na watu waliomchagua.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) , Abdallah  Bulembo (katikati) akizungumza na waandishi habari juu ya uchaguzi wa jumuiya ya wazazi leo katika makao makuu ya jumuiya hiyo leo jijini Dar es Salaam.kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Seif Shaaban Mohamed Bara na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi Bara, Barhan Abdul Ruta.