WAWEKEZAJI katika sekta ya kilimo na mifugo wamelalamikia ushindani unaoletwa na bidhaa kutoka nje kutokana na serikali kushindwa kuzidhibiti kwa njia ya kupunguza kodi na tozo mbalimbali katika uzalishaji.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana wawekezaji hao ambao pia ni sehemu ya wabia wa Kituo cha Kuendeleza Kilimo Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Kilimo, Mifugo, Maji na Umwagiliaji katika Kongani ya Ihemi mkoani Iringa na Njombe, walisema ipo haja serikali ikaangalia suala hilo kwa jicho pana ili kulinda bidhaa za ndani.

Mkurugenzi wa kiwanda cha maziwa cha ASAS Dairies Limited kilichopo mkoani hapa, Bwana Fuad Abri alisema haiwezekani Tanzania iwe nchi ya pili kwa idadi ya ng’ombe barani Afrika baada ya Ethiopia lakini bado inapitwa katika uzalishaji na uingizaji maziwa nchini.

“Wenzetu Kenya wanazalisha lita 1,500,000 za maziwa kwa siku lakini Tanzania inazalisha lita 120,000 kwa siku. Wakati huohuo sisi tunawapita kwa umbali katika idadi ya ng’ombe, kama hiyo haitoshi bidhaa za maziwa kutoka mataifa jirani zinaingia kwa wingi na kutoa ushindani mkubwa na bidhaa za ndani,” alisema Bw. Abri.

Alisisitiza kuwa zipo namna nyingi za kuzuia ushindani huu kwa sababu Serikali ya Kenya inashirikiana kwa kiasi kikubwa na wazalishaji maziwa na ndiyo maana wana uwezo wa kusafirisha nje kwa bei shindani.

“Katika biashara hii ya maziwa kitu kikubwa kinachotakiwa kuangaliwa ni namna gani unapata maziwa yako, bei utakayonunulia ikupe faida lakini faida yenyewe iwe katika soko shindani,” alisema Bw. Abri.
 Mkurugenzi wa kiwanda cha maziwa cha ASAS Dairies Limited mkoani Iringa, Bwana Fuad Abri akitoa mada juu ya uendeshaji wa kiwanda chake na ubia wao na Kituo cha Kuendeleza kilimo Nyanda za juu kusini mwa Tanzania (SAGCOT) alipotembelewa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Kilimo,Mifugo , Maji na Umwagiliaji. Lengo la ziara ya Kamati hiyo ni kujionea na kujifunza juu ya Kongani ya Ihemi na shughuli za SAGCOT.
Mkurugenzi wa kiwanda cha maziwa cha ASAS Dairies Limited, Bwana Fuad Abri (kulia)akitoa maelekezo ya uendeshaji wa kiwanda chake alipotembelewa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Kilimo,Mifugo , maji na umwagiliaji. Ikiwa ni sehemu ya ziara ya kamati hiyo kujionea na kujifunza juu ya kongani ya Ihemi na shughuli mbalimbali za Mpango wa Kuendeleza Kilimo Nyanda za juu kusini mwa Tanzania(SAGCOT). Wapili kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni mbunge wa Maswa Magharibi, Bwana Mashimba Ndaki. Watatu kulia ni Mjumbe wa kamati ambaye pia Mbunge wa viti Maalum Bibi Khadija Hassan Aboud. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT , Bwana Geoffrey Kirenga.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...